Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mbappe amekuwa na wakati mzuri kwenye kikosi cha PSG na klabu nyingi kubwa barani Ulaya zimekuwa zikihusishwa na kuitaka huduma zake ikiwamo Liverpool. Hata hivyo, kinachosubiriwa ni kwa klabu yenge nguvu na Madrid inaonekana itaishinda vita hiyo.
 
AMEZEEKA? Unacheza wewe! Cristiano Ronaldo bado yupo sana, kama unabisha nenda katazame staili aliyoanza nayo mwaka 2020.
Amewapiga Cagliari bao tatu ‘hat-trick’ akiiongoza Juventus kushinda kwa mabao 4-0 na kuthibitisha kuwa umri wa miaka 34 kwake ni namba tu, lakini haumzui kuendelea kuzitesa timu anazokutana nazo.
 
Kwa Ronaldo hat-trick yake ya juzi ilikuwa ni ya 56 na kumfanya akae juu kwenye orodha ya wachezaji wenye hat-trick nyingi zaidi kwenye soka.
Lakini, si Ronaldo pekee ndiye fundi wa kupiga tatu tatu, kuna mastaa wengine ambao ukikaa vibaya kukupiga hat-trick kwao ni kitu cha kawaida sana.
 
Sergio Aguero 17
Huyu ndiye anashikilia rekodi ya kufunga hat-trick nyingi zaidi 11 kwenye Ligi Kuu England, idadi sawa na gwiji wa Newcastle United, Alan Shearer. Kwa ujumla Aguero ana hat-trick 17 ambazo amezifunga akiwa na Atletico Madrid, Manchester City na Timu ya Taifa ya Argentina.
 
Screenshot_20200119-091435_Facebook.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Robert Lewandowski 19
Katika pambano la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu dhidi ya Red Star, Lewandowski aliweka rekodi ya kufunga mabao manne ya haraka zaidi, akifanya hivyo ndani ya dakika 14 na sekunde 31, wakati Bayern Munich ikishinda mabao 6-0. Kwa jumla straika huyu wa kimataifa wa Poland amefunga jumla ya hat-trick 19, akiwa na timu yake ya taifa, Borussia Dortmund na Bayern Munich.
 
Luis Suarez 29
Suarez alifunga hat-trick yake ya kwanza akiwa na jezi za Barcelona, mwaka 2015 wakati timu hiyo ilipoipiga Cordoba kwa mabao 8-0, lakini tangu wakati huo amekuwa mchezaji muhimu kwenye safu ya ushambuliaji ya Barca sambamba na Lionel Messi. Hadi sasa Suarez ana jumla ya hat-trick 29, idadi ambayo ameipata akiwa na jezi za Barca, Liverpool, Ajax na Timu ya Taifa ya Uruguay.
 
Lionel Messi 53
Messi anaongoza kwa kupiga hat-trick nyingi zaidi kwenye Ligi Kuu Hispania (La Liga) akiwa amepiga jumla ya hat-trick 35, moja zaidi ya Ronaldo mwenye umri wa miaka 34, na kwa ujumla Messi amepiga hat-trick 53, huku 47 akizipiga kwenye mechi za mashindano na 6 akipiga katika mechi za kirafiki na hat-trick hizo amezipata akiwa na kikosi cha Barcelona na timu ya Taifa ya Argentina.
 
Cristiano Ronaldo 56
Moja ya rekodi ambayo Ronaldo anamzidi Messi ni hii ya kufunga hat-trick 56, lakini kinachonogesha zaidi rekodi hii ni kwamba amefunga hat-trick hizi kwenye michuano 10 tofauti ambayo ni Serie A, La Liga, Ligi Kuu England, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la Mfalme, Kombe la Dunia la Klabu, Kombe la Dunia, Kufuzu Kombe la Dunia, Kufuzu Euro na UEFA Nations League, lakini pia Ronaldo ameungana na Alexis Sanchez kufunga hat-trick kwenye ligi tatu kubwa duniani ambazo ni La Liga, Ligi Kuu England na Serie A
 
Back
Top Bottom