Cristiano Ronaldo 56
Moja ya rekodi ambayo Ronaldo anamzidi Messi ni hii ya kufunga hat-trick 56, lakini kinachonogesha zaidi rekodi hii ni kwamba amefunga hat-trick hizi kwenye michuano 10 tofauti ambayo ni Serie A, La Liga, Ligi Kuu England, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la Mfalme, Kombe la Dunia la Klabu, Kombe la Dunia, Kufuzu Kombe la Dunia, Kufuzu Euro na UEFA Nations League, lakini pia Ronaldo ameungana na Alexis Sanchez kufunga hat-trick kwenye ligi tatu kubwa duniani ambazo ni La Liga, Ligi Kuu England na Serie A