Hati zilizovuja zinaonyesha jinsi mwanamke tajiri barani Afrika alivyopata utajiri wake kupitia unyonyaji kwa nchi yake na ufisadi. Isabel dos Santos alipata mikataba ya faida kubwa inayojumuisha ardhi, mafuta, almasi na simu wakati baba yake alipokuwa rais wa Angola, nchi iliyoko kusini mwa Afrika yenye utajiri wa maliasili. Hati hizo zinaonyesha jinsi yeye na mumewe walivyoruhusiwa kununua mali za serikali katika safu ya mikataba mibaya. Hata hivyo ameendelea kukana shutuma hizo akidai ni uwongo na kwamba kuna uwindaji wa kisiasa dhidi yake. Kwasasa amefanya Uingereza kuwa ndio makazi yake na anamiliki mali ghali katikati mwa London