Bale kuondoka Bernabeu
Kwa misimu mitatu sasa mfululizo, supastaa wa Wales, Gareth Bale amekuwa akidaiwa kwamba anaondoka Real Madrid. Maisha yake magumu chini ya kocha Zinedine Zidane pamoja na mashabiki wa Los Blancos kushindwa kumkubali, Bale muda wote amekuwa akivumishwa kwamba anataka kuondoka Santiago Bernabeu na kumfanya ahusishwe na timu kibao ikiwamo Manchester United, Tottenham Hotspur na hata kwenda China. Hii ni habari isiyokauka kila dirisha la usajili linapofunguliwa, kinachosikika kuhusu Bale ni kwamba ataondoka Real Madrid.