Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Marcus atakaa nje kwa muda atakaotaka yeye," alisema Solskjaer. "Hatutaki kuhatarisha maisha yake kwa sababu ya kuwa majeruhi. Wakati atakaporudi atakuwa fiti kwa asilimia 100%."
 
Solskjaer alilaumiwa na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na England, Ian Wright kwa uamuzi wa kumchezesha Rashford katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Wolves kwenye Uwanja wa Old Trafford wakati akijua ni majeruhi.
 
Kila dirisha la usajili linapofunguliwa unakutana na taarifa hizo na pengine hata katikati ya msimu, unasikia mchezaji fulani anatakiwa na timu fulani au ataondoka timu hii kwenda ile, lakini jambo hilo wala halikamiliki.
 
Hata baada ya dirisha la usajili kufungwa, bado jina la Mreno huyo lilikuwa linaendelea kuishi huko Old Trafford hadi hapo ilipofika Januari, ambapo mambo yalikolezwa zaidi na kudaiwa kwamba zimebaki hatua chache sana kabla ya kiungo huyo fundi wa mpira kwenda kuvaa jezi za Mashetani Wekundu. Lakini, hili ni jambo linaloishia midomoni tu, Bruno bado yupo Ureno.
 
Kabla hata Paul Pogba hajaondoka Juventus kurudi zake Manchester United, timu aliyokuwa akihusishwa kwamba angekwenda kujiunga ni Real Madrid. Kuna wakati ilifikia kuripotiwa kwamba hata Florentino Perez alikuwa ameshakamilisha baadhi ya mambo ili kumsajili kiungo huyo Mfaransa akakipige Bernabeu.
 
Kwenye dirisha la mwaka jana mambo ndiyo yalichachamaa zaidi hadi Januari hii, zimekuwapo taarifa za kwamba Barcelona wanajiandaa kumrudisha kikosini Mbrazili huyo. Bila shaka hata kwenye dirisha la usajili mwisho wa msimu huu, Neymar ataendelea kuhusishwa na mpango wa kurudi Nou Camp.
 
Dybala kuhama Juve

Kwenye dirisha hili la Januari 2020, hadithi bado ni zilezile za Paulo Dybala kuripotiwa kwamba ana mpango wa kuondoka Juventus. Dybala amekuwa akiripotiwa anaachana na Juventus tangu Cristiano Ronaldo alipojiunga na timu hiyo ya Turin.
 
Dybala kuhama Juve

Kwenye dirisha hili la Januari 2020, hadithi bado ni zilezile za Paulo Dybala kuripotiwa kwamba ana mpango wa kuondoka Juventus. Dybala amekuwa akiripotiwa anaachana na Juventus tangu Cristiano Ronaldo alipojiunga na timu hiyo ya Turin.
 
Bale kuondoka Bernabeu

Kwa misimu mitatu sasa mfululizo, supastaa wa Wales, Gareth Bale amekuwa akidaiwa kwamba anaondoka Real Madrid. Maisha yake magumu chini ya kocha Zinedine Zidane pamoja na mashabiki wa Los Blancos kushindwa kumkubali, Bale muda wote amekuwa akivumishwa kwamba anataka kuondoka Santiago Bernabeu na kumfanya ahusishwe na timu kibao ikiwamo Manchester United, Tottenham Hotspur na hata kwenda China. Hii ni habari isiyokauka kila dirisha la usajili linapofunguliwa, kinachosikika kuhusu Bale ni kwamba ataondoka Real Madrid.
 
Ronaldo kurudi Man United

Pengine hadi hapo atakapoamua kustaafu soka ndipo habari hizi za kumhusu Cristiano Ronaldo kurudi Manchester United zitazimwa. Miaka kadhaa iliyopita, wakati akiwa Real Madrid kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, supastaa huyo wa Kireno aliporudi kucheza dhidi ya Man United, jina lake lilihusishwa na timu hiyo hadi hapo alipohamia Juventus, bado fowadi huyo anahusishwa na mpango wa kurudi Old Trafford.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…