DADA YANGU AMENIAMBUKIZA UKIMWI NA HATAKI TENA KUNISAIDIA. Mimi ni Binti wa miaka 23, ni mwanafunzi wa mwaka watatu chuo, nilikua naishi kwa dada yangu ambaye ndiyo alianza kunisomesha tangu nilipomaliza kidoago cha sita baada ya wazazi wangu kufariki. Baada ya kuja kwa dada iniliona tabia mbaya za shemeji, alikua hahudumii chochote, anampiga sana dada na kila kitu anafanya dada, mpaka ada za watoto, shemeji alikua akimuomba pesa akikataa anampiga. Nilikaa nikiwa chuo mwaka wa kwanza mwishoni mwishoni shemeji alikuja kwangu, akaanza kuniambia ni kwanini anampiga dada yangu, alikua ananiambia kuwa anmapigakwakua dadayangu ni mkorofi, kiburi na ni mchawi anamloga ndiyo maana hafanikiwi. Aliniambia mambo mengi ya Dada ambayo yalinifanya ni mchukie dada,a kaniambia anataka kutoa pesa lakini dada yangu hataki kwani ni mchawi. Nilijikuta nakua karibu na shemu mpaka tukaanzisha mahusiano, akawa ananipenda ikafikia hatua tunafanya mambo waziwazi, dada alijua tukawa tunagombana lakini shemeji ndiyo alikua ni kila kitu akawa anampiga ananyamaza. Sasa mwaka jana mwezi wa nane nilipata ujauzito, shemeji aliniambia nibebe mimba kwani ananipenda na anataka mtoto na mimi. Kweli nilibeba mimba, lakini nilipoenda kupima kiliniki nikaambiwa kuwa nimeathirika hivyo nianze kutumia dawa, nilichanganyikiwa ila nilipomuambia shemeji hakujali. Nilimuambia dada akaishia kuniambia kuwa mbona yeye kaathirika muda tu anatumia dawa shemeji ndiyo aligoma kutumia dawa.