Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wolves - mechi 31, pointi 47

Ni kitu kingine kinachoshangaza kwamba Man United chini ya Ole imezidiwa pointi hadi na Wolves, ambapo ndani ya muda huo imecheza mechi 31 kwenye ligi na kuvuna pointi 47. Wolves katika mechi zake hizo, imeshinda mara 12, sare 11 na vichapo vinane, huku ikiwa imefunga mabao 43 na kuruhusu wavu wake kuguswa mara 40. Msimu huu, Wolves ipo kwenye nafasi ya saba, wakiwa pointi sawa na Man United, 34, lakini hiyo ilikuwa kabla ya mchezo wao wa jana Alhamisi usiku ambapo walitarajia kuwakabili Liverpool uwanjani kwao Molineux.
 
Crystal Palace - mechi 32, pointi 46

Ni rahisi kusema kwamba Man United iliamua kujizika yenyewe ilipochukua uamuzi wa kumpa kibarua cha kudumu Solskjaer. Kwa takwimu za kuanzia Machi mwaka jana, United imevuna pointi chake kuliko Crystal Palace, ambapo kikosi hicho cha Selhurst Park kimevuna pointi 46 katika mechi 32. Katika mechi hizo, Palace ilishinda 12, sare 10 na vichapo 10, huku ikiwa na mabao ya kufunga 37 na kufungwa 40. Jambo hilo linadhihirisha wazi kwamba Man United inajikaba kwa Ole.
 
Tottenham - mechi 32, pointi 44

Tangu ya muda ambao Solskjaer amekuwa kocha wa Man United, Spurs imekuwa chini ya makocha wawili, Mauricio Pochettino na sasa Jose Mourinho. Ndani ya muda huo, Spurs imecheza mechi 32 na kuvuna pointi 44, ambapo imeshinda 12, sare nane na vichapo 12 huku ikifunga mabao 48 na kufungwa 39. Msimu huu, Spurs ikiwa chini ya Mourinho inapambana kuhakikisha inaingia kwenye Top Four, vita ambayo inamkabili pia Solskjaer huko Old Trafford kama kweli anahitaji kulinda kibarua chake akiponyeka kwa sasa.
 
Everton - mechi 31, pointi 44

Mambo ya huko Goodison Park si haba. Kwa muda wa kuanzia Solskjaer alipopewa kazi huko Man United, Everton yenyewe imecheza mechi 31 na kuvuna pointi 44 ikiwa ni nyingi kuliko ilizovuna Mashetani Wekundu ndani ya muda huo. Katika mechi hizo, Everton, ambayo kwa sasa inanolewa na Mtaliano Carlo Ancelotti imeshinda mechi 12, sare nane na vichapo 11, huku ikifunga mabao 39 na kufungwa idadi hiyo hiyo ya mabao 39. Kwa msimu huu, Everton wamezidiwa pointi nne tu na Man United.
 
Man United - mechi 32, pointi 42

Chini ya Solskjaer inapitia kwenye majanga mengi kwelikweli. Baada ya kocha huyo kuonyesha makali alipokuwa wa mpito, mambo yalibadilika kuanzia Machi 28 mwaka jana, alipokabidhiwa mikoba ya kudumu ya kuinoa timu hiyo. Ndani ya muda huo, Man United imecheza mechi 32 kwenye ligi na kuvuna pointi 42, ambapo wameshinda mechi 11, sare tisa na vichapo 12, huku wakifunga mabao 43 na kufungwa 43. Hizo ni rekodi za hovyo kwa timu ya daraja la Man United kwamba tangu wakati huo wamepoteza mechi nyingi kuliko walizoshinda.
 
Arsenal - mechi 32, pointi 40

Pengine Arsenal ndio timu pekee, ambayo Solskjaer anaweza kujivunia kwamba tangu apewe kazi ya kudumu huko Man United timu yake imevuna pointi nyingi kuliko wabeba hao wa Emirates. Ndani ya muda huo, ambapo Arsenal imekuwa chini ya makocha wawili, Unai Emery na Mikel Arteta, imecheza mechi 32 na kuvuna pointi 40. Katika mechi hizo, Arsenal imeshinda 9, sare 13 na vichapo 10, wakifunga mabao 42 na kufungwa 46. Timu nyingine zilizovuna pointi 40 ndani ya muda huo ni Southampton, Burnley na Newcastle United.
 
Mimi nabisha[emoji23][emoji23][emoji23]
Mna uhakika gani km haikueditiwa?

Huu ushahidi Ni batili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] itakua unatokea kigoma weweView attachment 1333037
Yesu wangu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Umewaonea watu wa kigoma.
Acha kulinganisha watu wa kigoma na vitu vya ajabu.

Hivi unawajua waha wewe!?[emoji1787]


Nina wasiwasi umenichezea mchezo hapa[emoji848]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yesu wangu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Umewaonea watu wa kigoma.
Acha kulinganisha watu wa kigoma na vitu vya ajabu.

Hivi unawajua waha wewe!?[emoji1787]


Nina wasiwasi umenichezea mchezo hapa[emoji848]
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kakuchezea aliyekuquote
 
Aaah wapi itakua mahodaw huyo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Nilishaona nimeanza kufanyiwa mazigaombwe hapa[emoji848]
Nina wasiwasi na wewe [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Mimi Kwenye huo Uzi nilifikaje kwani?
Kuna kitu hapa sio bure[emoji23][emoji23][emoji23]

BTW,jina si langu jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kakuchezea aliyekuquote
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]dah

Jamani jina si langu,Mimi nitaandamana humu ndani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]dah

Jamani jina si langu,Mimi nitaandamana humu ndani

Sent using Jamii Forums mobile app
Stella bana[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…