SITI BINTI SADI.
Akiwa Nyota wa kwanza mkubwa wa kurikodi Taarab tokea miaka ya mwanzo ya santuri, Siti aliweza kuifanya Taarab kuwa maarufu kutokana na muziki wake mtamu na nyimbo za mapenzi zilizobeba ujumbe wa nguvu za kijamii na uchambuzi wakisiasa. Jambo moja lililoifanya kazi yake kuwa ya kiharakati ni vile kuimba kwake kwa kutumia lugha ya watu wa kawaida. Baada ya kuishi kwa muda mrefu katika mitaa ya Ng'ambo mjini Zanzibar, baadaye Siti alitembelea nchi mbali mbali za Afrika ya Mashariki akiimba na kuuza rekodi zake. Lililompa umaarufu zaidi miongoni mwa watu ilikuwa ni muziki mpya uliorekodiwa katika lugha yao wenyewe. Baada ya wasomo wanadai kuwa rekodi hizi za zamani zilichangia sana kuieneza lugha ya Kiswahili.
Akiwa mtoto wa watumwa, Siti alianza maisha kwa akali ya kitu, lakini kwa juhudi yake mwenyewe na sauti yake ya ajabu, aliweza kwanza kuimba taarabu ya kawaida, baadaye katika makasri na kumsifu Mfalme, na hata kuimba kwa Kiarabu. Baadaye aliigeuza midundo na mifumo ile ya kishairi na kuwa katika vinanda vya kawaida. Matokeo yake, Taarab ya Kiswahili ilimfanya awe Nyota na yeye kuifanya taarab iwe aina ya sanaa ambayo bado ni maarufu visiwani na isiyokosekana katika harusi na sherehe zote za Kizanzibari ..
View attachment 1337557