SHEIKH ABDALLA SALEH FARSY
Alikuwa ni mfano wa karne ya Ishirini, katika safu ndefu ya Ulamaa wa Kiislam kutoka Zanzibar. Mchango wake maarufu katika uislamu ni kuchapisha QUR'AN TAKATIFU, yenye kurasa 807, ambayo ni tafsiri ya mwanzo kamili inayokubalika katika lugha ya Kiswahili Sheikh Abdulla Saleh Farsy vile vile alikuwa kabobea katika sarufi ya Kiarabu. Akiwa katika umri wa miaka ya ishirini, alikuwa anaandika mashairi kwa kiarabu, jambo linaashiria ukubwa wa kiwango cha elimu ambacho ulamaa wa Zanzibar walikuwa wanasambaza nyakati zile.
Sheikh Abdulla aliteuliwa kuwa Mkaguzi Mkuu wa shule za msingi za Unguja na Pemba mnamo mwaka 1949, Mkuu wa Shule ya Lugha ya Kiarabu mwaka 1957 na Kadhi Mkuu wa Zanzibar mwak 1960. Aliondoka visiwani baada ya Mapinduzi ya 1964 na akafia Omani Novemba 9 mwaka 1982.
View attachment 1337555
hivi aliondoka kwa hiari au alifukuzwa?
moudgulf