Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Winga huyo matata ametua Wolves akitokea Olympiacos huku dili lake likifanyika siku ya mwisho ya kufungwa dirisha la usajili Ijumaa iliyopita. Wolves imemnasa mchezaji mwenye kipaji kikubwa, lakini hakujaliwa urefu, mchezaji huyo ni mfupi kwelikweli, anaitwa andunje.
 
Podence anaposimama kimo chake ni mita 1.6 (futi 5 na inchi 3), jambo linalomfanya kuwa mchezaji mfupi zaidi kwenye Ligi Kuu England kwa sasa. Hata hivyo, Podence si mchezaji pekee kwenye ligi hiyo mwenye kimo kidogo baada ya kuwamo wengine kibao. Hawa hapa andunje wanaotamba kwenye Ligi Kuu England kwa sasa.
 
Michael Obafemi – mita 1.69

Staa wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland, Michael Obafemi bado anawewa kukua kutokana na kwamba hajafikisha umri wa miaka 20. Hata hivyo, kimo chake hakijaonekana kuwa tatizo huko Southampton akipiga soka liliwakosha kocha na mashabiki wake. Kocha Ralph Hasenhuttl ameonyesha imani kubwa na Obafemi akionyesha kiwango baada ya kurudi uwanjani akitokea kwenye majeraha ya misimu na sasa ameongezwa kwenye kikosi cha kwanza.
 
N’Golo Kante –mita 1.68

N’Golo Kante anabaki kuwa mmoja kati ya viungo mahiri kabisa wa kukaba kwenye Ligi Kuu England na dunia kwa ujumla. Shughuli yake matata ndani ya uwanja imemfanya Kante kuzipa ubingwa wa Ligi Kuu England, Leicester City na Chelsea alipozichezea timu hizo katika kipindi cha misimu miwili mfululizo. Kante ni mmoja kati ya wachezaji wachache walioshinda ubingwa wa Ligi Kuu England misimu miwili mfululizo wakiwa na timu mbili tofauti. Umbo halijawahi kuwa tatizo kwake.
 
Lucas Torreira – mita 1.68

Kwa urefu wa futi tano na nusu, Lucas Torreira wakati huo asingehesabika kuwa mmoja kati ya viungo moto wa kati katika zama za zamani za Ligi Kuu England walipokuwa wakicheza kina Patrick Vieira kurudi nyuma. Lakini, tangu zama hizo zilipopita, wamekuja viungo wengi wa kati akiwamo Kante na Claude Makelele, ambao walifungua njia ya viungo wenye vimo vidogo kutamba kwenye ligi. Torreira anapiga mzigo huko Arsenal na shughuli yake si mchezo ndani ya uwanja bila ya kujali kimo chake ni mita 1.68 tu.
 
Nampalys Mendy – mita 1.67

Karibu miaka minne iliyopita, Leicester City ilivunja rekodi yao ya uhamisho wakati ilipovamia huko Nice na kumsajili Nampalys Mendy kwa ada ya Pauni 13 milioni. Kiungo huyo panga pangua alikuwa hakosi kwenye kikosi cha Leicester City msimu wa 2018/19, laakini baada ya hapo mambo yamekuwa magumu baada ya ujio wa Brendan Rodgers huko King Power. Msimu huu ameanzishwa kwenye mechi mbili tu, lakini hilo halitokani na kimo chake kwa sababu shughuli yake ndani ya uwanja si mchezo.
 
Aaron Lennon –mita 1.65

Aaron Lennon amekuwa akiwaburudisha mashabiki wa Ligi Kuu England kwa zaidi ya miaka 10 sasa licha ya kiwango cha soka lake kuonekana kufifia miaka ya karibuni. Kwa sasa anakipiga huko Burnley baada ya kutamba na timu za Tottenham Hotspur na Everton. Kwenye kikosi cha Burnley, Lennon hapangwi sana pengine ni kutokana na kutokuwa mmoja kati ya watu wanaoingia kwenye staili ya uchezaji ya timu hiyo kutumia nguvu nyingi ndani ya uwanja. Kocha Sean Dyche amekuwa hampangi mara kwa mara.
 
Christian Atsu –mita 1.65

Christian Atsu amechezea timu nne kwenye Ligi Kuu England na baada ya kukosa namba kwenye kikosi cha kwanza huko Stamford Bridge alitimkia zake St James’ Park katika majira ya kiangazi ya mwaka 2017. Baada ya kutulia kwa muda mrefu kwenye kikosi cha Newcastle United, staa huyo wa kimataifa wa Ghana amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kikosi hicho kuwa chini ya Kocha Steve Bruce. Uamuzi huo haukuwashangaza mashabiki wa Newcastle, lakini kila kitu kinabaki palepale kuwa Atsu ni mmoja kati ya wachezaji wenye vimo vidogo waliopo kwenye Ligi Kuu England kwa sasa.
 
Ryan Fraser –mita 1.63

Ryan Fraser ndiye namba mbili kwa ufupi Ligi Kuu England baada ya Podence. Staa huyo ameanza kucheza kwenye ligi tangu mwaka 2015 na ameonyesha kiwango kikubwa licha ya kuwa na kimo kifupi. Kwa msimu huu mambo yake si mazuri, amefunga mabao matatu na asisti moja tu, wakati msimu uliopita asisti na mabao kwa pamoja vilikuwa 21. Lakini, Fraser, anayecheza pembeni bado amekuwa tishio kwa wachezaji wa timu pinzani kutokana na uwezo wake mkubwa wa kumiliki mpira na kasi uwanjani. Huduma yake anatoa huko Bournemouth na wapinzani wanaisoma namba.
 
Kabla ya mechi hiyo kupigwa, kipa Dragowski aliambia Corriere dello Sport: “Nimemsoma Cristiano Ronaldo, najua anavyopiga mashuti yake. Siwaambii jinsi gani anavyopiga penalti zake la sivyo atabadili upigaji wake. Ningependa ziwepo penalti kwenye mchezo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…