Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Glaucoma ni nini?
hili ni ongezeko la presha ya macho, kimsingi macho hua yana presha ya 10mmhg mpaka 21mmhg lakini inapozidi hapo mgonjwa hutambulika kama mgonjwa wa presha ya macho.
mara nyingi ugonjwa huu hurithiwa na hauonyeshi dalili zozote mpaka baadae sana mtu anapokua mtu mzima.
 
nini chanzo cha presha ya macho?
kitaalamu upande wa mbele ya jicho kuna maji maji kitaalamu tunaita aquous homour ambayo kazi yake ni kuleta virutubisho kwenye sehemu za jicho kama iris, lenzi na cornea pia kuondoa mabaki ya matumizi ya virutubisho hivyo lakini pia hutunza shepu ya jicho sasa maji maji haya yanapozidi ndio presha ya macho inapanda
 
kwa kawaida hali hii hurithiwa kutoka kwenye kizazi kimoja mpaka kingine na sababu zingine zinazoweza kuongeza presha hii ni magonjwa ya macho, kuumia jicho kwa kupigwa na kitu au kumwagikiwa na kemikali au baada ya upasuaji wa macho wa kutibu tatizo lingine la macho.
 
watu gani wako kwenye hatari ya kuugua ugonjwa huu?


  • watu ambao ukoo wao una wagonjwa wa hivyo
  • watu wenye kisukari
  • watu wenye umri zaidi ya miaka 40
  • watu walioumia macho
  • watu wanaotumia dawa fulani fulani kama predinisolone
  • watu waliopata ajali na kuumia macho
  • watu wasioona vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…