Kijana mmoja alikua mtu wa hasira sana, kila mara alikua akimpiga mke wake na hasira zilipoisha basi alimuomba msamaha. Mke wake alikua akilia sana lakini kwakua alikua akimpenda basi alikua akimsamehe. Alivumilia sana na kulalamika kwa watu lakini kila mara yule kijana alikua akisema kuwa nitabadilika lakini alikua habadiliki. Siku moja alikuja mzee mmoja kuwatembelea, aliona ile hali na alipoongea na yule kijana alisema anataka kubadililika lakini hawezi kuzizuia hasira zake. Mzee alimuambia subiri, alienda dukani na kununua kilo kumi za misumari, alirudi na kumkabidhi yule kijana. Kisha akamchukua na kumpeleka katika nyumba kubwa iliyokua imetelekezwa haijamalizika kujengwa. Katika ile nyumba kulikua na ukuta mkubwa wa mbao. Yule Mzee alimuambia kuanzia leo kila ukipatwa na hasira kabla ya kufanya kitu chochote, chukua nyundo na hii misimari na njoo ugongee msumari mmoja hapa. Badala ya kumpiga mke wako basi njoo gongea msumari mmoja hapa kisha rudi nyumbani basi ndiyo dawa yake. Kijana alishangaa lakini alikubaliana na yule Mzee. Siku iliyofuata alipata hasira, badala ya kumpiga mkewe alikumbuka maneno ya Mzee, alichukua mfuko wake wa misumari na kuongozana mpaka kwenye ukuta wa mbao na kugongea msumari mmoja kisha akarudi. Hasira zilipompanda alifanya hivyo hivyo, siku ya kwanza alijikuta kagongea misumari ishirini. Kila mara alpokua akitembea na misumari mizito alikua akiwaza kuhusu hasira zake, alikua akichoka na hivyo kila siku alipunguza hasira zake mpaka akaweza kuzicontrol na akawa haendi kugongea tena misumari, hasira zimemuisha. Alienda kwa yule Mzee na kumuambia kuwa nimeshamaliza, sina hasira tena. Yule Mzee alichukua alimuambia basi kama kashamaliza basi aende kuing’oa ile misumari yote. Kijana alifanya hivyo na alipomuambia Mzee alisema twende sasa ukaone. Walifika katika ule ukuta wa mbao na Mzee alimuuliza kijana unaona nini? Kijana aliangalia na kuona matundu ya misumari, ukuta ulikua umeharibika na una matobo mengi.