moudgulf
JF-Expert Member
- Jan 23, 2017
- 159,165
- 777,891
Nimejifunza.
Namshukuru Mungu kwa kunijaalia moyo wa subira.
Namshukuru Mungu kwa kunijaalia moyo wa subira.
Mzee alimuuliza umejifunza nini kijana alinyamaza bila jibu ndipo yule Mzee alipomuambia. Katika maisha unapochukua kisu na kumchoma mtu kisha ukakitoa hata kama huyo mtu akikusamehe lakini bado tobo la kisu litaendelea kubakia tu. Ingawa umetoa misumari yote katika huu ukuta wa mbao lakini bado unaona kuna matundu, wewe umeondoka na misumari yako lakini umeuachia ukuta matundu na kamwe hautarudi katika hali ya kawaida. Hivyo hivyo, unapotaka kumpiga mkeo basi kumbuka huu ukuta kuwa, hata kama utakuja kumuomba msamaha na kukusamehe lakini maumivu, kuvunjika moyo na makovu kamwe hayawezi kuisha. Nirahisi wewe kusema nisamehe kama ilivyorahisi wewe kung’oa misumari lakini kwake ni ngumu kuzima matundu ya maumivu uliyomsababishia hivyo kila siku kumbuka kuwa anakusamehe lakini bado anabaki na matundu. Kijana aliondoka akiwa amejifunza kitu, alirudi na kumuomba tena mkewe msamaha na kila mara hasira zilipompanda alijizuia, alikumbuka mashimo aliyoyaacha kwenye ukuta na kuzuia hasira zake. Hakumpiga tena mkewe, kila alipokosea walieleweshana kama watu wazima, hapo alijikuta anafuraha zaidi na mkewe wanaelewana zaidi akimsikiliza kuliko kipindi kile alivyokua anampiga. KAMA UMEMUELEWA MZEE BASI