Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tim Berners-lee huyu ni mtaalam wa kompyuta huko London uingereza huyu mtu alizaliwa mwaa 1955

huyu mtu anajulikana kwa kuanzisha kitu kinachoitwa [[World Wide Web]] yani [[WWW]] intanet ya dunia nzima

1991 Berners-lee alikuwa mtaalam wa kompyuta kwenye CERN {Taasisi ya kinyukria ya ulaya}

kwa kazi hii alikuwa baba wa wavuti

leo hii anaishi marekani akiwa profesa katika chuo kikuu cha MIT mjini boston

Berners-lee alishirikiana na Robert Cailliau kuanzisha WWW

Robert Cailliau alizaliwa mwaka 1947 huko ubelgiji

mpaka sasa Cailliau anaumri wa miaka 73 na Berners-lee anamiaka 64

hawa waanzirishi wa World Wede Web....WWW
 
Simuungi mkono Magufuli katika kauli na matendo mengi hasa ya kikatili, Lakini kwa hili la kutokwenda kumzika muuaji Moi, big up. Labda atapunguza dhambi zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je, umeshawahi kujiuliza unacheka vipi na kwa nini? Kila mmoja wetu ameshawahi kucheka au kulia, labda tu kama ana tatizo. Kucheka na kulia inatazamwa kama vitu muhimu sana katika jamii yoyote kwa kucheka au kulia, mwili hufanya mabadiliko ambayo ni muhimu sana kwetu binadamu. Kucheka na kulia ni kama sifa za lazima kwetu katika kutufanya tuishi tukiwa na afya pamoja na maisha marefu.
 
Machozi ya kihisia yana kemikali na homoni, ambazo zinapopunguzwa mwilini humfanya mliaji kujihisi vizuri. Ndiyo maana inashauriwa kwamba, mtu anapokuwa kwenye uchungu fulani, akilia, aachwe alie tu. Baada ya kulia, mtu hujisikia kufarijika kiasi.
 
Kuna mambo ambayo yanakubalika katika jamii au jamii zote kwamba, mtu anapolia hakuna wa kumshangaa. Mambo kama misiba, simanzi na mengine ya aina hiyo. Iliaminika na inaaminikia kwamba, mtu asipolia wakati akiwa kwenye maumivu hujiumiza. Ni kweli kujiumimza kwa sababu anashindwa kupunguza hisia hizo za maumivu. Huu ni ukweli wa kisayansi na ndiyo maana katika jamii nyingi, kulia sana baada yakufia kwa mfano kama ni lazima.
 
Uzoefu wa maisha na mapenzi ni sababu nyingine ambazo zinaruhusiwa na jamii kumfanya mtu kulia. Wanawake wameruhusiwa au kufanywa na jamii kulia zaidi. Lakini faida za kulia zinashauri kwamba, mwanamume ndiye ambaye angetakiwa kulia zaidi kuliko mwanamke.
 
Kila jamii kwa mila na desturi zake, au mazoea yake, zimeruhusu kulazimika mtu kulia kwa simanzi au maumivu. Lakini pia jamii hizo zimeweka mipaka au masharti ya wapi na wakati gani mtu alie. Kwa baadhi ya jamii, umewekwa muda maalum wakulia kwenye misiba. Kwa mfano, baadhi ya jamii, kulia kwa sababu ya kifo cha mtu huruhusiwa hadi saa nne na baada ya hapo mkuu wa jamii hiyo hutangaza kwamba, msiba huo ulitokea miaka minne iliyopita na haruhusiwi mtu tena kulia tena.
 
Kama ilivyo kulia, kucheka pia kumewekewa vigezo na mipaka na jamii. Kitu ambacho kinaonekana ni cha kuchekesha Tanzania kwa mfano, kinaweza kisiwe cha kuchekesha huko au mahali pengine Duniani. Jamii pia hupanga ni mahali na kitu gani ambacho kwacho, mtu anaruhusiwa kucheka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…