Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jumapili ya Februari 11, 1990 Dkt. Ouku aliishangaza familia yake baada ya kumwona akihudhuria kanisani. Alisali katika Kanisa la “African Inland Church” AIC, lililopo kijijini kwake huko Koru. Siku hiyo Ouko alihubiri mwenyewe na kisha kuomba sana Kanisa limuombee.
 
Baada ya kumaliza kupiga injili kanisani wiki hiyo Dkt. Ouko alimfuata Mzee Mwai Kibaki ili amuombee msamaha kwa Mzee Nyayo (Moi) lakini ilishindikana pia. Maombi na sala za jumapili hazikushika, Dkt. Ouko alimwendea tena adui yake mkubwa, Hezekiah Oyugi, safari hii akamwomba ampatie gari la Serikali ili atoroke nchini, naye Oyugi akakubali. Lakini Februari 12, 1990 Dkt. Ouko alikatiwa mawasiliano.
 
Alfajiri ya Jumanne, Februari 13, 1990; Gari nyeupe aina ya Mercedes Benz kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Nyanza, ilifika nyumbani kwa Dkt. Ouko huko Koru alikoamriwa kwenda. Watu waliokuwemo ndani ya gari hilo walijitambulisha na kudai walitumwa na Rais Moi kumfuata kwa ajili ya “Wito maalum”. Muda si muda wakafika watu wengine 15 wakiwa katika gari la Serikali.
 
Baada ya Ugeni huo wa watu 15 kuwasili nyumbani hapo, walinzi binafsi wa Dkt. Ouko walifukuzwa na kuonywa wasizungumze kitu. Palepale Dkt.Ouko akajua sasa za kufa kwake zimewadia. Akawaomba watekaji wake arudi ndani kubadili nguo.

Baada ya Dkt. Ouko kuruhusiwa kuingia ndani, akaamua kuandika majina ya watu aliowafahamu katika kundi lile. Haraka haraka Ouko akachukua kalamu na karatasi na kuandika “Oyugi, Biwott, Koba, Koskei na Noah Too”, kisha akaipachika karatasi yenye majina hayo nyuma ya fremu ya picha yake kubwa ya ukutani.
 
Baada ya kumaliza kilichompeleka ndani na kutoka nje, palepale Dkt. Ouko alikamatwa, akafungwa kamba na pingu kama kibaka, akarushwa kwenye buti la gari ya Mercedes Benz kama mzigo, kisha safari yake ya kuondoka Duniani ikaanza, msafara ule ulielekea Ikulu, baada ya kufika Ouko akatolewa kwenye buti na kutupwa sakafuni kama gunia la viazi, Ouko akilia sana kama mtoto huku akiomba msamaha kwa kosa asilolijua.
 
Ouko aliteseka na kulia Sana kwa maumivu na uchungu wa kuvunjwa viungo vyake kwa kipigo, na kisha Waziri mwenzake (Inaelezwa ni Nicholas Biwott) akatoa bastola na kumtandika risasi ya kichwa na kumuua palepale. Daktari Ouko akakata roho na kufa, kisha akafungashwa kwenye magunia na safari ikaendelea lakini safari hii kwa kutumia usafiri wa ndege ya jeshi. Walipokaribia nyumbani kwake kijijini Koru jirani kidogo na shamba lake, mwili wake ulitupwa chini na kuchomwa moto.

1581595340432.png
 
Breaking News: shocking

UN publishes 1st quarter Demography Report 2019

There are 7.8Billion people on planet . (earth).
The report shows

Women = 5.6Billion
Men = 2.2Billion


So, they advised women to be careful in showing attitudes to any man because out of the 2.2 Billion men:

• One billion are married already.
• 130 million are in prison.
• 70 million are mentally ill.

That means that we have just about 1 billion men available for marriage and out of the
1billion:

• 50% are jobless
• 3% are gay
• 5% are Catholic Priests
• 10% are your relatives
• 32% are above 66years

So, ladies both the married and singles, you have to rethink before treating any man like trash.

For details visit UN demography report


AISEEE HIZI RESEARCH BUANA NI SHIDA
 
Back
Top Bottom