Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nyumba ni choo asikuambie mtu..


Kwema bro? Hope uzima utakuwepo pande hizo, tumshukuru Mungu kwa kutuweka hai hadi dakika hii.

Mungu ni mwema siku zote!!

Sikuiona hii bro. Hekaheka zilinizidia...

Yote uliyosema ni kweli japo nimeona mpendwa wako eti anakwesheni.

Tumshukuru Mungu kwa yote na tumuombe Aendelee kutulinda [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
[emoji1][emoji1]
 
Binadamu tunaweza kuwa tunaona kitu kimoja kwa namna tofauti kabisa , hii inatokana na kutofautiana mitazamo tu au yaweza kuwa ni kutokana na vitu ambavyo tumejifunza na kuzisikia sana, ndiyo vitu ambavyo tumeaminishwa kuwa vipi hivyo.
 
Hata akitokea mtu wa kutuelewesha au kutuambia kitu kipya tunakuwa hatupo tayari kujifunza hicho, hata tukisikiliza hatusikilizi kwa lengo la kujifunza au kuelewa bali tunasikiliza tu ili tuelezee msimamo wetu , tunavyoelewa sisi.
 
Si jambo baya kuelezea kile unajua au kuelewa lakini ni vizuri kama utakuwa tayari pia kujifunza vitu vipya, naamini mwanafunzi hachagui nini afundishwe au asikie, lakini akifundishwa kama hajaelewa huuliza maswali kwa nia ya kueleweshwa zaidi na si kwa nia au lengo la kubishana.
 
Tukiangalia katika wakati tulionao wa maendeleo ya sayansi na teknolojia, kuna vitu vingi vizuri sana tu lakini vipo na vibaya vilivyokuja na hii teknolojia, Hivyo kwa sababu hizo nilizosema mwingine anaweza kuona kuwa kukua kwa teknolojia kuna madhara sana, hakufai, mfano huu utandawazi wengi wanauona kama jambo baya lisilofaa kabisa, na wengi wanatumia nguvu nyingi sana kujaribu kufanya kila mtu aone kuwa ni kitu kisichofaa kwa jamii, na wanaposema hivi wana sababu za msingi za kuamini wanavyoamini,
 
maana kuna mambo mengi yasiyofaa yanaendelea mitandaoni, watu wanaiga mambo yasiyofaa humo na hata maadili ya jamii yanamomonyoka, lakini kwa kuwa tu wapo wanaoona hivyo haimaanishi kwamba ni kweli utandawazi ni mbaya na hauna faida, zipo faida nyingi tu za utandawazi ikiwa utautumia vizuri unaweza kunufaika sana tu.
 
Wapo watu wengi wamefaidika sana na mitandao hii ya kijamii kwa kukutana na watu wapya ambao wamewafundisha vitu vingi, watu wamenufaika kiroho na hata kijamii kwa namna ambavyo wametumia mitandao hii ya kijamii,
 
maana kupitia hii hauhitaji kuonana na mtu ili muweze kufundishana au hata kujadilia baadhi ya mambo, pia inasaidia hata kutunza muda na hata gharama za kukutana au kumfuata mtu mahali fulani kwa ajili ya majadiliano, naweza kuwa hospitali, barabarani na nikasoma vizuri au hata kuhudhuria mafundisho au hata ibada bila shida kabisa.
 
Pia katika maisha haya iwe kazini , nyumbani au popote ulipo unaweza kukutana na mtu akakuambia kuwa mtu fulani ni mbaya sana au ana sifa hizi na hizi na pengine akakupa mabaya tu ya huyo mtu, akajitahidi kukuelezea na kukufanya umuone mtu huyo hafai kabisa katika jamii, au hafai kuwa rafiki yako kabisa na pengine si mtu hata wa kufanya naye biashara n.k,
 
Sasa hapo ni wajibu wako wewe kama mtu unayejielewa na kuelewa kuwa sisi binadamu hatupo kama watu wanavyosema tupo, au kwa kuwa fulani ameniona mimi sifai au mimi ni mzuri haimaanishi kwamba kila mtu ataniona hivyo, hivyo hata kama umeambiwa nini kuhusu mtu fulani hebu usiende kwake ukiwa na hiyo picha uliyopewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…