Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Usilazimishe ndoa yako iwe kama ya fulani maana wao wana kanuni zao ambazo labda wewe huziwezi. Jambo muhimu ni ninyi kujijengea ndoa yenu yenye sera zitakazowapa amani, upendo na kumpa Mungu utukufu. Usiseme ningepata mume/mke kama wa fulani mambo yangekuwa safi maana hujui mwenzio amechuchumilia kiasi gani (ambacho wewe hujachuchumilia kwa mwenzi wako) mpaka ukamuona yule mwenzi wake ni mfano wa kuigwa. Mungu amekupatia mwenzi wa kufanana naye ni wajibu wako katika hadhina ya kufanana kwenu ilipo na uifuate.
 
Samehe mara kwa mara
Wahenga walisema kuishi na watu kazi. Hivyo ni muhimu kuelewa jinsi ya kuishi nao, uelewe kwamba hakuna mtimilifu na kila siku yupo ambaye atakukosea ama kukukwaza. Unaweza ukajikuta unakosa furaha kila siku sababu ya kubeba uchungu na maumivu yaliyotokana na watu waliokukosea.
 
Mafanikio siyo ufunguo wa furaha. Furaha ni ufunguo wa mafanikio. Kama unapenda unachokifanya, utafanikiwa. Mojawapo ya siri ya kufanikiwa na kuwa na furaha katika kile unachokifanya, ni kwa kupenda kile unachokifanya.
 
Back
Top Bottom