Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1582740588608.jpeg
 
STRAIKA, Alexandre Lacazette ana makubaliano na klabu ya Arsenal kwamba watamruhusu aondoke kwenye timu hiyo kama watashindwa kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
 
Lakini, kikosi hicho cha kocha Mikel Arteta hakijapoteza mchezo wowote yangu mwaka huu wa 2020 uanze, hivyo jambo hilo linawapa matumaini na nguvu ya kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.
 
Manchester City amefungiwa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa misimu miwili na kama watafeli kwenye rufaa yao basi jambo hilo litafanya timu itakayomaliza nafasi ya tano kupata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kama chama la Pep Guardiola kumaliza msimu ndani ya Top Four.
 
Lakini, Arsenal wanaweza kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2020-21 kama watabeba ubingwa wa Europa League, ambako wamejiweka kwenye nafasi nzuri ya kutinga hatua ya 16 bora baada ya kuwachapa Olympiacos 1-0 ugenini.
 
Mechi 5 zijazo za Arsenal
Leo, Alhamisi vs Olympiacos - nyumbani
Machi 2 vs Portsmouth - ugenini
Machi 7 vs West Ham - nyumbani
Machi 14 vs Brighton - ugenini
Machi 22 vs Southampton - ugenini
 
Back
Top Bottom