Na mara nyingi watu wengi wamekuwa wakivutwa chini na watu walioamua kuwaona kama walivyokuwa jana, walioshindwa kukubali na mtu wanayemuona leo, na wanajitahidi hata kuwashawishi watu wengi waamini wakuhukumu leo kwa ile jana yako. Kwa dunia yetu wengi ni wepesi wa kuamini vile ulivyokuwa jana kuliko ulivyo leo, mtu anaweza kukubali aliyoambia kuhusu jana yako leo, kuliko wewe anayekuona leo, anaamua na kuchagua kukuona hivyo, inachukua muda watu hawa kuja kukuelewa.
Kitu cha msingi katika maisha haya ni vyema kuishi vile ulivyo leo, usiishi ili kuwafanya watu fulani wakukubali au kukuelewa, ishi wewe ulivyo leo hata kama wapo wengi wanaokuona kivingine au walioshikilia jana yako, usiwaangalie hao, bali wewe endelea kuishi maisha yako, kufanya yale unayafanya kwa usahihi ili mradi haumkosei muumba wako na wala hauvunji sheria za nchi, maana ni ngumu kubadili watu wanavyokuona na kukutafsiri lakini ikiwa unaishi uhalisia wako, hauigizi , watakuelewa tu hata kama ni baada ya muda mrefu.