LIONEL Messi ni shida. Lakini, Pierre-Emerick Aubameyang, Kylian Mbappe, Mohamed Salah, Sergio Aguero na Robert Lewandowski nao ni moto wa kuotea mbali.
Hapo achana na Cristiano Ronaldo, Neymar, Luis Suarez na Ciro Immobile, ambao shughuli yao imekuwa si ya kitoto kwenye uhusika katika mabao mengi kwa takwimu za kuanzia Agosti 2017.
Hapo achana na Cristiano Ronaldo, Neymar, Luis Suarez na Ciro Immobile, ambao shughuli yao imekuwa si ya kitoto kwenye uhusika katika mabao mengi kwa takwimu za kuanzia Agosti 2017.
Ukiwekewa orodha ya washambuliaji hatari kwenye kuhusika katika kuzipatia mabao timu zao ndani ya muda wa miaka isiyozidi mitatu, masupastaa hawa 10 ndio kiboko yao.
Messi ameonyesha ni balaa zaidi, ambapo katika mechi 90 alizocheza ndani ya muda huo amefunga mabao 98 na kuasisti mara 37, hivyo kwa ujumla wake akiwa amehusika kwenye mabao 125. Ndio mechi 90, mabao 125. Hiyo ndio hatari ya Messi.
Ciro Immobile anawatikisa watu akilingana na Mo Salah, ambapo wawili hao kila mmoja amehusika kwenye mabao 92. Immobile amecheza mechi 94, amefunga mabao 71 na kuasisti 21 wakati Mo Salah amecheza mechi 97, amefunga mabao 68 na kuasisti mara 24.
Straika wa Bayern Munich, Lewandowski anafuatia akiwa amehusika kwenye mabao 88 katika mechi 86 alizocheza ambapo amefunga mabao 76 na kuasisti 12, wakati staa wa Juventus, Ronaldo amehusika na mabao 83 ndani ya muda huo, ambapo amecheza mechi 79, akifunga mabao 68 na kuasisti 15.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.