Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nilikuwa na mambo yangu katika baa," Bon Jovi alisema. "Na timu hiyo ilikuwa hapo usiku wa kuamkia jana (Jumatatu) na kwa jinsi-- kwa kutumia nguvu ya whiski na bia-- walivyoizidi nguvu Chelsea, inatoa picha pia kuhusu tabia ya unywaji kwa Chelsea."
 
Katika mchezo huo, Bayern ilijipatia mabao yake katika kipindi cha pili kupitia kwa Serge Gnabry aliyefunga mawili na la tatu likiwekwa wavuni na Robert Lewandowski.
Timu hizo zitarudiana Machi 18 kwenye Uwanja wa Allianz Arena
 
Arsenal walitupwa nje usiku wa jana katika mashindano ya Europa Ligi baada ya kukumbana na kipigo cha mabao 2-1 wakiwa nyumbani kwenye uwanja wao wa Emirates huku akishuhudiwa Aubameyang akipoteza nafasi ya wazi katika mchezo huo.
 
Youssef El-Arabi ndiye aliyezamisha jahazi la Arsenal katika uwanja wao wa nyumbani baada ya kufunga bao la pili kwa Olympiacos dakika ya 120, ndani ya dakika 90 za kawaida washika mitutu wa London walifungwa bao moja hivyo ilibidi wakaamuliwe dakika 30 kwani mchezo wa kwanza, walishinda bao 1-0 nchini Ugiriki.
 
Aubameyang, ambaye mchezo huo alifunga bao la kufutia machozi kwa Arsenal licha ya kupoteza nafasi ya wazi, msimu uliopita alitwaa tuzo ya kuwa mfungaji bora wa msimu wa Ligi Kuu England 'EPL' na Mohamed Salah na Sadio Mane wa Liverpool kila mmoja akipachika mabao 22.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…