Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Kitu cha kushangaza watu niliowataja hapo juu ni watu wa kwanza kulaumu viongozi na serikali kwa ujumla kuwa imekosa uaminifu, wanasahau kwamba nao ni sehemu ya serikali, wanasahau kwamba nao popote pale walipo wana wajibu wa kuwa mawakili wa uaminifu, wanatakiwa kuwa waaminifu popote pale walipo haijalishi ni eneo gani, pale utakapokuwa mwaminifu kuna mwingine atajifunza kitu kwako, wapo utakaowafanya wajione kuwa nao wana wajibu katika hilo, watagundua kuwa hao watu waaminifu wanatengenezwa kuanzia huku majumbani mwetu, jiulize kama wewe si mwaminifu je wanao watakuwaje? Jiulize ni mbegu gani unapanda kwa jamii inayokuzunguka?