Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kitu cha kushangaza watu niliowataja hapo juu ni watu wa kwanza kulaumu viongozi na serikali kwa ujumla kuwa imekosa uaminifu, wanasahau kwamba nao ni sehemu ya serikali, wanasahau kwamba nao popote pale walipo wana wajibu wa kuwa mawakili wa uaminifu, wanatakiwa kuwa waaminifu popote pale walipo haijalishi ni eneo gani, pale utakapokuwa mwaminifu kuna mwingine atajifunza kitu kwako, wapo utakaowafanya wajione kuwa nao wana wajibu katika hilo, watagundua kuwa hao watu waaminifu wanatengenezwa kuanzia huku majumbani mwetu, jiulize kama wewe si mwaminifu je wanao watakuwaje? Jiulize ni mbegu gani unapanda kwa jamii inayokuzunguka?
 
Unaweza kuamua kuanzia leo, kutimiza majukumu yako kwa uaminifu hata kama hakuna mtu anayekuomba ripoti, ni kwa faida yako ndugu, amua leo kuwahi kazini, ukifika fanya kazi kwa uaminifu, achana na mipango isiyo ya kiaminifu maana inakufanya uishi kwa wasiwasi na siyo salama kwa afya yako pia, ukiacha mbali hasara nyingine nyingi tu.
Anza wewe kuwa mwaminifu na wengine watajifunza kwako.
 
Wewe bana, sasa sisi WAGUMU maabara za kufanyia vitendo vya hizi nadharia tutazipata wapi? aah! 😀😀😀🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Duuu jamani jamani, si kwa kufunguka huku.
Ulisema unaishi vile?[emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…