Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

464135562_551009.jpg
 
Matatizo ya mabeki

Wakati Barcelona imekuwa ikifunga sana tu msimu huu, tatizo lao kubwa ni safu ya ulinzi, imeshindwa kabisa kutengeneza ukuta imara. Barca ndiyo timu ya juu iliyoruhusu mabao mengi zaidi msimu huu.
 
Setien habadiliki

Pale Bernabeu, kulikuwa na kocha mmoja ambaye aliweza kusoma mchezo na kufanyia kazi makosa kupitia kubadili mbinu na kufanya mabadiliko, huyu ni Zinedine Zidane wa Real Madrid. Baada ya Madrid kubadilika kipindi cha pili Setien alichelewa sana kufanya mabadiliko kuendana na kasi ya mchezo.
 
Umakini hakuna

Ili kucheza vizuri katika mfumo wa Setien, Barcelona inahitaji kuwa makini sana ikiwa na mpira mguuni haitakiwi kupoteza pasi mara kwa mara, pia wanatakiwa kucheza pasi za haraka na hilo lilikosekana Bernabeu.
 
Kiwango cha Messi

Messi hajawa kwenye kiwango bora katika siku za karibuni. Japokuwa bado anaongoza mbio za kuwania kiatu cha dhahabu Hispania, lakini Barcelona inapata shida anapokuwa hana siku bora uwanjani.

Kitendo cha Marcelo kufanikiwa kumkimbiza na kumpora mpira ni ushahidi tosha kwa sasa hayuko kwenye ubora wake.
 
Jurgen Klopp amesema matokeo ya jana usiku iliyopata Liverpool dhidi ya Chelsea hayajamuumiza.

Kocha huyo alisema alipata maumivu baada ya kupoteza mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Watford.

Kauli ya Klopp imekuja baada ya Liverpool kufungwa mabao 2-0 na Chelsea katika mchezo wa Kombe la FA.

Mabao ya Ross Barkley na Willian yalitosha kuendeleza kipigo kwa timu hiyo katika mechi tatu kati ya nne za mwisho ilizocheza hivi karibuni.
 
Back
Top Bottom