Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Inawezekana kutokana na kutokufanya mazoezi ya kutosha au hawa wachezaji wa kufanya hivyo. Barca ilishikwa na kigugumizi kila ilipoanzia mpira chini kutoka kwa Marc-Andre ter Stegen na Real Madrid wakatumia nafasi.
 
Matatizo ya mabeki

Wakati Barcelona imekuwa ikifunga sana tu msimu huu, tatizo lao kubwa ni safu ya ulinzi, imeshindwa kabisa kutengeneza ukuta imara. Barca ndiyo timu ya juu iliyoruhusu mabao mengi zaidi msimu huu.
 
Setien habadiliki

Pale Bernabeu, kulikuwa na kocha mmoja ambaye aliweza kusoma mchezo na kufanyia kazi makosa kupitia kubadili mbinu na kufanya mabadiliko, huyu ni Zinedine Zidane wa Real Madrid. Baada ya Madrid kubadilika kipindi cha pili Setien alichelewa sana kufanya mabadiliko kuendana na kasi ya mchezo.
 
Umakini hakuna

Ili kucheza vizuri katika mfumo wa Setien, Barcelona inahitaji kuwa makini sana ikiwa na mpira mguuni haitakiwi kupoteza pasi mara kwa mara, pia wanatakiwa kucheza pasi za haraka na hilo lilikosekana Bernabeu.
 
Kiwango cha Messi

Messi hajawa kwenye kiwango bora katika siku za karibuni. Japokuwa bado anaongoza mbio za kuwania kiatu cha dhahabu Hispania, lakini Barcelona inapata shida anapokuwa hana siku bora uwanjani.

Kitendo cha Marcelo kufanikiwa kumkimbiza na kumpora mpira ni ushahidi tosha kwa sasa hayuko kwenye ubora wake.
 
BARCELONA imepania kuimarisha safu yake ya ushambuliaji katika usajili wa majira ya kiangazi na straika wa Inter Milan, Lautaro Martinez, ndiyo anaongoza orodha ya wachezaji ambao wanasakwa na miamba hiyo Nou Camp.
 
Jurgen Klopp amesema matokeo ya jana usiku iliyopata Liverpool dhidi ya Chelsea hayajamuumiza.

Kocha huyo alisema alipata maumivu baada ya kupoteza mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Watford.

Kauli ya Klopp imekuja baada ya Liverpool kufungwa mabao 2-0 na Chelsea katika mchezo wa Kombe la FA.

Mabao ya Ross Barkley na Willian yalitosha kuendeleza kipigo kwa timu hiyo katika mechi tatu kati ya nne za mwisho ilizocheza hivi karibuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…