Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sasa wakati Pep Guardiola na jeshi lake wakirudi tena Old Trafford leo Jumapili, Solskjaer anaamini vijana wake wamejifunza kwa makosa waliyoyafanya na hawatatoa book tena zaidi ya kupambana kupata ushindi.
 
Wakati mwingine unapokuwa nyumbani mbele ya mashabiki zako unatakiwa kuwaonyesha ubora kwa kumfunga mpinzani wako, hilo ndio tulilifanya na ndani ya dakika 20 tulijiachia na hapo wakatuadhibu kwa kufunga mabao ya haraka haraka.
 
Halikuwa tatizo kubwa, lakini lilituondoa mchezoni kabisa na hapo City wakajenga ujasiri. Kama sasa hivi wameshinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Real Madrid pale Bernabeu (Ligi ya Mabingwa Ulaya), wamebeba taji la Ligi hivyo, watakuja hapa wakiwa na ujasiri na watacheza mchezo wao ule ule,” aliongeza Ole.
 
Wakati Ole akitaka kusaka alama tatu muhimu pale Old Trafford ili kufukuzia kumaliza ndani ya nafasi nne za juu ili afuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, tisho la kukosekana kwa nyota hao linamuweka roho juu.
 
Mbali na hao ambao wamepata majeraha hivi karibuni, Ole amekuwa akisaka ushindi kwenye mechi nyingi bila huduma ya kiungo ghali wake Paul Pogba na straika Marcus Rashford ambao wako nje ya uwanja kwa muda mrefu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…