Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Aguero akikabiliana na shabiki uwanjani
Manchester City ilipata pigo iliopoteza kwa Wigan Athletic katika kombe la FA mwezi Februari 2018.
Baadhi ya mashabiki waliingia uwanjani baada ya mechi na mambo yakawa mabaya kati ya shabiki mmoja wa City na mshambuliaji Sergio Aguero.
Picha za runinga zilimuonyesha Aguero akimsukuma shabiki mmoja huku mshambuliaji huyo wa Argentina akisema baadaye kwamba alitemewa mate na kutukanwa.
Wigan walipigwa faini ya £12,500 kwa kuruhusu mashabiki kuingia uwanjani hatua iliopelekea mashabiki wengine kurarua matangazo na kuwatupia maafisa wa polisi waliokuwa uwanjani.
Aguero alikwepa adhabu kutoka kwa shirikisho la soka nchini England.
 
Kandarasi ya Patrice Evra na klabu ya Ufaransa ya Marseille ilikuwa fupi kufuatia hatua yake ya kumpiga teke kichwani shabiki mmoja.
Kabla ya mechi ya kombe la Yuropa dhidi ya Vitoria Guimares , kanda ya video ilimuonyesha Evra na wachezaji wengine wakikimbia katika tangazo moja ambapo baadhi ya mashabiki walikuwa wamekaribia uwanjani.
Evra alimpiga teke mmoja wa mashabiki katika kichwa na akaonyeshwa kadi nyekundu.
Alipigiwa marufuku na Uefa kutoka katika michezo yake kwa miezi saba na kuamua kuondoka Marseille kwa makubaliano baada ya kujiunga na klabu hiyo ,mwezi Januari 2017.
 
Cantona alikuwa mfano mzuri kuwahi kuonekana.
Mwezi Januari mwaka 1995, mchezaji huyo aliushangaza ulimwengu wakati aliporuka katika eneo la mashabiki na kumpiga teke shabiki mmoja wa Crystal Palace aliyekuwa amekaa katika eneo la mbele la mashabiki katika uwanja wa Selhurst Park, akimuudhi.
Cantona alikuwa amepewa kadi nyekundu muda mfupi uliokuwa umepita na alipokuwa akielekea kutoka uwanjani , alijibu matusi aliokuwa akipokea kutoka kwa shabiki wa Palace Matthew Simmons.
Alipigwa marufuku ya miezi tisa na shirikisho la soka la FA na kukiri kumpiga shabiki huyo.
Hukumu yake ya kuhudumia wiki mbili jela ilibatilishwa baada ya kukata rufaa na Cantona akajibu kwa kuviambia vyombo vya habari kwamba ''Mabata mzingi yanapofuata boti ya kuvua samaki hudhania kwamba '' dagaa watatupwa baharini''.
 
KOSA #1:Kunyoa punde tu tunapo ingia bafuni.
Tunajua tuna haraka,lakini haraka hizi hupelekea maumivu makali ya kunyoa.Tufanye kunyoa ni jambo la mwisho baada ya kukoga miili yetu.Hii husaidia nywele hizo kua laini vyema kunyolewa nakupunguza uwezekano wa kuumiza ngozi <skin allergic>.
 
KOSA #1:Kunyoa punde tu tunapo ingia bafuni.
Tunajua tuna haraka,lakini haraka hizi hupelekea maumivu makali ya kunyoa.Tufanye kunyoa ni jambo la mwisho baada ya kukoga miili yetu.Hii husaidia nywele hizo kua laini vyema kunyolewa nakupunguza uwezekano wa kuumiza ngozi <skin allergic>.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…