Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Katika mechi ya kwanza walikosa wachezaji wengie sana kutokana na majeraha, kiasi cha kumtumia Axel Tuanzebe kama beki wa kushoto katika mfumo wa 4-2-3-1, alifanya kosa baada ya kupiga pasi mbovu iliyonaswa na Bukayo Saka aliyemlisha Pierre-Emerick Aubameyang akafunga. Mechi ya pili ambayo walifungwa 2-0 pale Emirates ndiyo moja ya sababu timu kuhamia mfumo wa 3-5-2.
 
Hatari zote katika mechi hiyo zilitoka kwa Nicolas Pepe ambaye alimtesa sana Luke Shaw, katika mfumo wa 4-2-3-1 kutokana na Rashford kushindwa kushuka chini kumsaidia. Katika mechi zote mbili dhidi ya Arsenal beki ya kushoto ndiyo ilizidiwa
 
Mfumo huu unatumika kwa sasa kutokana na aina ya wachezaji waliopo, tangu atue Trafford, Bruno Fernandes amekuwa bora sana, hivyo kama timu hiyo itamnasa Jadon Sancho ambaye ataingia kwenye nafasi ya James, huku Rashford akiongoza mashambulizi mbele sehemu ambayo kwa sasa anatumia Anthony Martial na Jack Grealish ukitarajiwa kunogesa zaidi timu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…