Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jua linatazamiwa kufa kabisa baada ya miaka Bilioni 7-8 ijayo. Mfano kama litakufa kwa wakati huu, itatuchukua dakika 8 kuweza kugundua mabadiliko kadhaa. Baada ya hapo maisha kwa wanyama na mimea kadhaa haitakuwepo japo inakadiriwa baadhi ya mimea itaweza kudumu kwa muda. Baada ya miaka milioni 5 itamezwa kabisa.
 
Elon Musk' ana mpango wa kuleta huduma ya intaneti kwa unafuu zaidi. Mtumiaji utapata GB 300 pamoja na kupiga simu na kutuma meseji bure kwenda eneo lolote Duniani kwa sh 22,000 tu. Wastani wa kawaida GB 300 kupata itakubidi uwe na 300,000 Tsh. Usisahau mpango wake wa kupeleka watu kutalii sayari ya Mars' kuanzia mwaka 2020 unakuja.
 
"Furaha yako sio furaha yake. Jifunze kujipa furaha mwenyewe mwambie nae ajifunze kujipa furaha kwanza kisha mkutane wote kwa pamoja ili mfurahi. Usimpe mwenzako wajibu wa kukupa wewe furaha wakati wewe mwenyewe kujipa furaha umeshindwa huo ni Ubinafsi", Will Smith
 
Kuna muda Brazil hunyesha mvua ya Bui bui. Mwaka 2014 Sri-Lanka ilinyesha mvua ya samaki. Mwaka 2009 Ishikawa,Japan ilinyesha mvua ya Vyura. Sababu inasemekana ni kimbunga kidogo ambacho huchota viumbe hao na kuwatupa mbali kama mvua hivyo kuonekana kama wanatokea katika mvua.
 
Wafungwa nchini Ujerumani wanaruhusiwa kupika vyakula vyao, kuunda timu zao za mpira, kupamba vyumba vyao wanavyotaka, kucheza magemu, kuvaa nguo za kawaida, kutembelewa na wenza wao kwaajili ya huduma ya kimwili na kumiliki funguo za vyumba vyao. Wafungwa wanaonesha tabia nzuri zaidi huruhusiwa kwenda kutafuta kazi mtaani pia wanapewa ruhusa ya kutoka kwaajili ya matembezi ya mara kwa mara. Lakini kumbuka unaruhusiwa pia kutoroka sababu ni haki yako ila usiharibu mali yoyote ya gereza.
 
Wafungwa nchini Ujerumani wanaruhusiwa kupika vyakula vyao, kuunda timu zao za mpira, kupamba vyumba vyao wanavyotaka, kucheza magemu, kuvaa nguo za kawaida, kutembelewa na wenza wao kwaajili ya huduma ya kimwili na kumiliki funguo za vyumba vyao. Wafungwa wanaonesha tabia nzuri zaidi huruhusiwa kwenda kutafuta kazi mtaani pia wanapewa ruhusa ya kutoka kwaajili ya matembezi ya mara kwa mara. Lakini kumbuka unaruhusiwa pia kutoroka sababu ni haki yako ila usiharibu mali yoyote ya gereza.
 
Conrad Henri Roy III, alijiua akiwa na miaka 18 mwaka 2014 baada ya kushawishiwa na mpnz wake, Michelle Carter. Conrad na Michelle walikuwa wanasumbuliwa na msongo wa mawazo ambapo Conrad alikuwa anataka kujiua lakini anashindwa. Michelle alianza kumshawishi ajiue ili aachane na matatizo ya duniani. Hatimaye Conrad alijiua tarehe 13 July 2014 kwa gesi ya kabonimonoksaidi ndani ya gari lake. Michelle alishtakiwa na akafungwa lakini baadae aliachiwa kwa utetezi wa kuwa alifanya makosa akiwa na matatizo ya akili.
(Rolling Stones, Wikipedia, Quora
 
Kangaroo jike ana sehemu tatu za Uke'. Mbili kwaajili ya kubeba mbegu za dume ambae nae Dume katika uume wake umegawanyika sehemu mbili. Uke unaobaki ni maalum kwaajili ya kuzaa, kutokana na hilo Kangaroo Jike muda wowote anaweza kupata mimba akijamiiana.
 
Ulaji mara kwa mara wa Vitunguu Saumu' husaidia kuongeza hamu ya tendo la ndoa' kwa wanaume. Husaidia kulainisha mafuta yote yanayopatikana katika mishipa ya damu hivyo huongeza kasi ya mzunguko wa damu kwa haraka. Wakati wa tendo la ndoa damu huteremka kwa urahisi mpaka kwenye Uume' na kuzidi kuongeza hamu zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…