Difenda wa Austria David Alaba, mwenye umri wa miaka 27, anaangalia uwezekano wa kuondoka katika Bayern Munich huku Real Madrid na Barcelona wote wakimtaka. (Sport Bild - in German)
Manchester United wanaangalia uwezekano wa kumleta kikosini mshambuliaji wa zamani Eric Cantona, mwenye umri wa miaka 53 kuchukua cheo cha balozi. (Mirror
West Ham wanafuatilia kwa karibu maendeleo ya kimchezo ya difenda Muingereza Dion Sanderson, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo katika Cardiff kutoka Wolves. (Daily Mail)
Chelsea wamezungumza na Barcelona kuhusu uwezekano wa kusaini mkataba na kiungo wa kati Mbrazil Philippe Coutinho, mwenye umri wa miaka 27, kwa mkopo msimu ujao. (Sport, in Spanish)
Inter Milan wako tayari kumpa mkataba wa mwaka mmoja zaidi Muingereza Ashley Young, mwenye umri wa miaka 34, baada ya kuwafurahisha kimchezo tangu alipohamia kikosini mwezi Januari kutoka Manchester United. (Gazzetta dello Sport, in Italian)