Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pique alisema hayo kwa sababu aliamini Paris Saint Germain ilikuwa inataka Pesa ndefu sana kwa ajili ya Neymar na kama Barcelona ingekubali kulipa hiyo Pauni 200 milioni ambayo PSG walihitaji timu hiyo ingekutana na rungu la Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) kwa sababu wangevunja kanuni ya udhibiti wa matumizi ya kiungwana ya fedha.
 
Ndiyo, maana katika kipindi hiki kigumu Bodi ya Wakurugenzi ya Barcelona inaona ni bora kukaa chini na wachezaji wa klabu hiyo na kuwaeleza tatizo lililopo ili nao wachangie kitu kuhakikisha timu hiyo haikutani na mdororo wa uchumi.
 
Lakini, wakati Barcelona ikiendelea kufikiria njia nzuri ya kujinasua kwenye mtego huu wa kipato ilionasa, Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) na lile la Ulaya (Uefa) wanafikiria kuja na njia madhubuti ya kuokoa klabu ambazo zimeathiriwa sana na kusimama kwa msimu kutokana na janga la Corona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…