Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kale nilitembea
Nikilemewa dhambi
Nilikosa msaada
Kuniponya mateso


Hata nilipofika
Mahali pa msalaba
Palinifaa Sana
Sitasahau kamwe

Panapo msalaba
Kinatolewa cheti
Cha kuingia mbinguni
Kisicho Cha kanisa

Yule Bwana mjinga
Likwenda Bila cheti
Kitumai kuingia
Kama walionavyo

/Usifiwe msalaba
Lisifiwe kaburi
Linalozidi yote
Asifiwe Mwokozi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yesu kwetu Ni rafiki
Hwambiwa haja pia
Tukiomba kwa Babaye
Maombi asikia

Lakini twajikosesha
Twajitweka vibaya
Kwamba tulimwomba Mungu
Dua angesikia


Una dhiki na maonjo?
Una mashaka pia?
Haifai kufa moyo
Dua atasikia

Hakuna mwingine mwema
Wa kutuhurumia
Atujua tu dhaifu
Maombi asikia



Je,hunayo hata nguvu?
Huwezi kwendelea
Ujapodharauliwa
Ujarushwa pia

Watu wangekudharau
Wapendao dunia
Hukwambata mikononi
Dua atasikia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Twende kwa Yesu Mimi nawe
Njia atwonya tuijue
Imo chuoni na mwenyewe
Haya asema njoo

Wangojeani?Leo yupo
Sikiza Sana asemapo
Huruma Yake ikwitapo
Ewe kijana njoo

Wana na waje atatwambia
Furahini mkisikia
Ndiye mfalme wetu pia
Na atusihi njoo

/Na furaha tutaiona
Mioyo ikitakata Sana
Kwako mwokozi kuonana
Na milele kukaa

Nyimbo za kikristo
/Kweli tutaona furaha
Tukifika kwenye Raha kuu
Tukisafishwa mioyo yetu
Na Yesu mwokozi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sioshwi dhambi zangu
Bila damu yake Yesu
Hapendezewi Mungu Mungu
Bila damu yake Yesu

/Hakuna kabisa
Dawa ya makosa
Ya kututakasa
Ila Damu yake yesu

Sipati tumaini
Bila damu Yake Yesu
Wema Wala amani
Bila damu Yake Yesu

Sipati patanishwa
Bila damu Yake Yesu
Hukumu yanitisha
Bila damu Yake Yesu

Twaimba utukufu
Una damu Yake Yesu
Milele twaisifu
Hiyo damu Yake Yesu

/Hakuna kabisa
Dawa ya makosa
Ya kututakasa
Ila Damu yake yesu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu wimbo mkiuimba mpo wengi, sauti zimepangiliwa unaweza kudhani Yesu anashuka saa hiyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu amenihurumia
Tendo hili kubwa Sana
Sikustahili Jambo hili
Nimelipata bure tu

/ Sasa najua haya yote
Nasifu huruma yake

Nalistahili kupotea
Lakini naruhumiwa
Mungu amenipatanisha
Na Yeye kwa Yesu kristo

/Hivi vyatoka wapi
Nasema Ni huruma tu

Jambo hili lenye huruma
Nitalisifu daima
......
Hata ije siku ile....
Ya kuonana kwa Salama

/ndilo furaha yangu kubwa
Naingojea nikifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii haipo kwenye tenzi, labda kama imeongezwa sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…