Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

BOMU MWEZINI 2
Baada ya kuona mpinzani wake ameonesha mafanikio makubwa ya kuushangaza ulimwengu, Marekani akajawa na hasira iliyoambatana na wivu. Akataka 'kujibu mapigo'. Hatimaye tarehe 6 disemba 1957 akaandaa roketi iliyoitwa 'Vanguard TV3' kwa ajili ya kurusha satelaiti kwenye obiti.

Bahati mbaya akashindwa, baada ya chombo hiko kulipuka hata kabla ya kuruka mbali. Marekani hakukata tamaa, mwezi mmoja baadae yaani tarehe 31 januari 1958, akafanikiwa kurusha satelaiti iliyojulikana kama 'Explorer 1'. Miezi miwili baadae, marekani ikarusha tena satelaiti kwenye orbit, satelaiti hiyo inajulikana kama 'Vanguard 1'.

Duu!..Sasa hadi hapo tunaona ushindani kati ya urusi na marekani ukawa ni 'ngoma droo', kwakua wote walikuwa wameshatoshana uwezo.

Ndipo sasa Marekani ikaanza kufikiria ifanye nini ili dunia nzima ijue kwamba yeye ndio 'gwiji' wa maswala ya haya anga. Ndipo akaja na mpango alioupa jina la 'PROJECT A199'. Lengo la mpango huu likiwa ni kudondosha bomu la nyuklia katika mwezi ili mlipuko wake uweze kuonekana hadi huku duniani. Na hatimaye watu wote tuweze kushuhudia jinsi mwezi unavyowaka moto.

Kwa kufanya Hivyo, Marekani iliamini kuwa itatengeneza heshima duniani kote, hasa kwa wale mahasimu wake, Urusi. Ndipo jopo la wataalamu takribani kumi wakiongozwa na Leonard Reiffel, walikutana mjini Chicago katika chuo cha 'Illinois Institute of Technology' kujadili mustakabali wa bomu hilo wanalotarajia kulilipua mwezini
 
*BOMU MWEZINI - 2*

Mwezi mei 1958, jopo la wataalamu kumi wakiongozwa na *Leonard Reiffel* walikutana mjini Chicago katika chuo cha *Illinois Institute of Technology * kujadili mustakabali wa bomu hilo wanalotarajia kulilipua mwezini. Miongoni mwa wataalamu katika jopo hilo, alikuwepo mnajimu Gerard Kuiper pamoja na *Carl Sagan* ambao walipendekeza kutumia bomu la hydrogen. Pendekezo hilo lilipingwa na shirika la anga la marekani wakisema kuwa bomu la Hydrogen ni zito sana badala yake walipendekeza bomu aina ya *W25 warhead.*

Miezi michache baadae, *January 1959* mpango huo ulisitishwa, kutokana na kuhofia madhara ambayo yangetokea endapo zoezi hilo lisipofanyika kwa usahihi. Kwahiyo Marekani hawakuweza kutekeleza tukio hilo.

Ifahamike kwamba mpango huo ulikuwa ni siri iliyotunzwa kwa muda wa miaka karibia 45. Na ulimwengu umekuja kugundua uwepo wa mpango huo wa marekani Mwaka 2000, baada ya *Leonard Reiffel* kutoa siri hiyo.

Reiffel ndiye alikuwa kiongozi wa jopo hilo lililokuwa linaandaa mpango huo. Licha ya kuwa alivujisha siri hiyo mwaka 2000, serikali ya Marekani ilikanusha vikali kuwepo kwa mpango huo.
 
*Kumbe bwana!!*

Kipindi marekani inaandaa mpango huo urusi nao kumbe walikuwa wanajitayarisha kufanya hivyo hivyo, napo kwa usiri wa hali ya juu. Siri ambayo imedumu hadi mwaka 2010 pale kulipovuja nyaraka za siri zikionyesha kuwa urusi USSR nao walikuwa wanasuka mpango wa kurusha bomu huko mwezini. Tena inaonyesha urusi wao ndio walioanza kuandaa mipango hiyo hata kabla ya marekani.

Mpango huo wa urusi ulipewa jina la *Project E,* ikiwa imegawanyika katika vipengele vinne, E1 ikilenga kufika tu mwezini, E2 na E3 ikilenga kutuma chombo huko mwezini na kupiga picha dunia, na E4 ikilenga kudondosha bomu la nyuklia huko mwezini. Na wao pia hawakuweza kufanikisha mpango huo wakiohofia madhara ambayo yangeweza kutokea.

Naam, hiyo ndio *'Space Race',* ushindani wa teknolojia ya anga baina ya mahasimu wawili, USSR na Marekani.



Ila kufikia mwaka 1969, Marekani ikaonekana kuibuka mshindi katika ushindani huo baada ya kuandika historia ya kuwa nchi ya kwanza kupeleka binadamu mwezini. *Neil Armstrong*alikuwa binadamu wa kwanza kukanyaga mwezini.
#chakushangaza
 
Bro; basi juzi nikamuona dogo mmoja hapa anasukuma Rolls-Royce ukanijia akilini ghafla. Sijui kwa nini. Kama bado basi siku moja usukume ndinga kama hii bro. KD Himuselfu [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
View attachment 1399265
Rolls Royce..... Ooh Jizazi!

Vitu kama hivyo vimetengenezwa kwaajili ya kutumiwa na binadamu, na binadamu ni kama mimi na wewe japo inahitaji juhudi na jitihada sana kufika huko....

Muumba akabariki maono na hisia zako vikawe vya kweli kabisa siku moja na sisi tupush mali kama hizo. Ameen 🤲🏼🤲🏼
 
Mwanaume mmoja (Rajarao) mkazi wa Jimbo la Adhra Pradesh India, amepata kiharusi kufuatia mshtuko alioupata baada ya Mke wake mwenye umri wa miaka 73 kujifungua Mapacha wawili wa kike ambapo kabla ya hapo wawili hao hawakuwahi kubahatika kupata Mtoto maishani mwao.
 
🤣🤣🤣🤣🤣 Shame on Koreans
 
Robert G Heft, akiwa na umri wa miaka 17 mwaka 1958, aliibuni bendera ya Marekani inayotumika sasa hivi. Ubunifu huo ulikuwa sehemu ya kazi za mikono kwenye somo la stadi za kazi shuleni. Alipata "B-", lakini baada ya bendera hiyo kupitishwa kuwa bendera ya nchi, 1960, mwalimu wake alimuongezea maksi akampa "A".Chanzo:Wikipedia/Flag of the United States
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…