Usimwachie mtu nyaraka zakoKuna watu wanawaamini watu wengine kiasi cha kuthubutu kuwaachia nyaraka zao muhimu. Kumbuka mtu mwingine anaweza kupoteza au hata kuharibu nyaraka zako muhimu.
Nimeshuhudia pia baadhi ya taasisi au kampuni zikitaka kushikilia nyaraka muhimu za mwajiriwa kama vile vyeti vya taaluma ili asiache kazi kabla ya mkataba kwisha.
Ni muhimu Kuwa makini na taasisi au kampuni hizi kwani lolote linaweza kutokea na ukapoteza nyaraka zako.Neno la mwishoNi wazi kuwa mara nyingi umuhimu wa kitu haufahamiki hadi pale mtu anapokikosa kitu hicho. Kupoteza nyaraka muhimu ni jambo baya lenye usumbufu na changamoto nyingi.Hivyo ni vyema ukahakikisha unazingatia mambo yaliyoelezwa kwenye makala hii ili kuhakikisha usalama wa nyaraka zako muhimu.
Hakuna mtu anayependa kuwa na madeni, lakini mara nyingi watu hujikuta katika madeni makubwa. Kwa kiasi kikubwa watu wengi huingia kwenye madeni kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha matumizi kuliko kipato
Madeni siyo kitu kizuri hasa ikiwa hayatalipwa kwa wakati. Swala la kuepuka madeni ni swala linalohitaji maamuzi sahihi ya kifikra pamoja na mikakati stahiki.
Utawasikia watu wakikosoa bajeti ya serekali lakini hawana bajeti zao binafsi. Bajeti binafsi ni muhimu kwani hukuwezesha kupanga juu ya mapato na matumizi yako.
Kuna matumizi chungu nzima ya pesa, lakini matumizi ya lazima ni machache. Ikiwa kipato chako ni kidogo hakuna haja ya kufanya mambo kama vile kununua simu au nguo za gharama kubwa.
Nimeshuhudia baadhi ya watu wakikopa mikopo kwa ajili ya sherehe na matumizi mengine ya anasa. Mambo kama haya huwaingiza watu wengi kwenye madeni makubwa, hivyo yakupasa kuyaepuka.
Watu wengi hushindwa kurejesha mikopo kutokana na kukopa bila mpango. Inatakiwa kabla ya kukopa uhakikishe una mpango mzuri unaoonyesha jinsi utakavyotumia na kurejesha mkopo huo.
Kumbuka pesa ya mkopo hasa kutoka kwenye taasisi za kifedha inatakiwa irejeshwe kwa wakati tena kwa riba. Hivyo epuka kutumia pesa za mkopo bila mpango unaoeleweka vyema.
Watu wengi hutumbukia kwenye matumizi makubwa au yasiyo na ulazima kutokana na ushawishi wa marafiki kwenye matumizi yao ya pesa.
Hakikisha kila unachokinunua au kutumia pesa yako kina maana kwako na hakitakupotezea pesa zako. Kumbuka mrejeshaji wa mkopo ni wewe na wala siyo rafiki yako.
Kutumia vizuri huduma kama vile maji, simu, umeme, gesi au hata mafuta kutakuwezesha kuokoa kiasi kikubwa cha pesa. Kwa mfano hakuna haja ya kukopa kifurushi cha simu, ili tu kuchati au kumsalimia rafiki yako.
Hakikisha kila pesa unayoweka kwenye huduma haipotei. Hili litakuokolea pesa nyingi ambazo utazitumia kwa mahitaji mengine na kuepuka madeni.
Mara nyingi matumizi huwa makubwa kuliko kipato; na hii ndiyo sababu kubwa ya watu kukopa pesa. Hakikisha unajitahidi kutumia pesa kidogo kuliko zile unazozipata ili ujiwekee akiba na uweze kukidhi mahitaji yako ya msingi.
“Dawa ya deni ni kulipa.”
Kwa hakika dawa ya deni ni kulipa, tena kwa wakati na si kulimbikiza. Kutolipa deni kwa wakati hukufanya ujiwekee mzigo mkubwa mbeleni na wala si kupunguza chochote.
Inakupasa kulipa madeni kwa wakati, hasa madeni ya taasisi za kifedha kwani kutolipa kwa wakati kutakufanya uongeze riba ya mkopo zaidi.
Je umejiunga kwenye huduma kama vile bima au vifurushi vya televisheni visivyokuwa vya ulazima? Hakikisha huduma zote zinazokugharimu pesa ambazo si za lazima unaziepuka.
Kwa njia hii utaweza kupunguza matumizi yako na kuokoa pesa kwa ajili ya matumizi mengine, jambo hili litakuwezesha kuepuka kukopa.
Mara nyingi milango ya kutoa pesa ni mingi kuliko ile inayoleta pesa. Ni muhimu kutokutegemea chanzo kimoja cha pesa kwani kikikwama au kuzidiwa itakubidi ukope.
Hakikisha unabuni chanzo kingine cha pesa hata kama ni kidogo. Kumbuka “kidogo kidogo hujaza kibaba”.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.