Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kama wana elimu wanaweza kuwa wajenzi huru; lakini kama hawana elimu, hawawezi kuwa wajenzi huru.

Shetani ni mjanja sana. Anajua bila elimu hataweza kutawala dunia, baada ya mpango wa Mungu kukamilika. Anajua, mtu akipata elimu ni rahisi sana kujua kama Shetani hayupo. Hivyo Shetani atatimiza malengo yake bila watu kujua.
 
Mungu hatakubali kuwa na mtu katika ufalme wake ambaye hatakubali kutawaliwa naye. Usikubali kutawaliwa na Ibilisi, kubali kutawaliwa na Mungu. Ni jukumu letu kuanza kuishi sasa kama vile tutakavyoishi mbinguni. Shetani anataka uwe na hekima ya duniani ili akupumbaze. Lakini hofu ya Mungu ndiyo msingi wa hekima ya kweli. Ukitaka asikupumbaze, pokea roho ya Mungu kwa kubatizwa. Ukiipokea roho ya Mungu utajua mambo ya Mungu, ambayo dunia haiwezi kujua.
 
Usipoangalia kwa undani sana, Shetani anatutawala kwa sababu hatuna uwezo wa kumwona. Aidha, bila hata sisi kujua, anaweza kuwasiliana nasi kimawazo na kitabia kupitia hewa hiihii inayotusaidia katika kuishi.

Wengi katika dunia hii hawajui kama wanadanganywa au walishadanganywa tayari. Shetani hataki tujue kama anatudanganya au ameshatudanganya tayari, na hataki tujue kama yuko hapa kwa ajili ya kutudanganya sisi. Tunajua tu kwa sababu Neno la Mungu hudhihirisha ukweli huu kupitia Roho Mtakatifu na malaika wema, na tunauamini.
 
Watoto wadogo wanakufa. Watu wazima wasiokuwa na hatia wanakufa vitani na katika majanga mengine ya asili. Kwa nini? Watoto wadogo wanaokufa walikuja duniani kufanya nini?
Kwa nini watu wasiokuwa na hatia wanakufa ilhali Mungu yupo na asiwaepushe na matatizo ya dunia hii?
Kama aliweza kuzuia binadamu wasiishi majini kwa sababu watakufa kwa nini asizuie matatizo yasiwapate watoto na watu wazima wasiokuwa na hatia?
Sisi ni wadogo sana na Mungu ni mkubwa mno. Jibu hatutaweza kulielewa pamoja na kwamba tumepewa. Hata hivyo, Mungu hababaishwi na mwili. Anababaishwa na roho.
 
Adamu na Hawa walipotenda dhambi waligundua kuwa kumbe walikuwa na miili, walipogundua kuwa walikuwa uchi, kisha Mungu akawalaani. Miili yao ikakosa thamani mbele ya Mungu, sisi wote tukalaaniwa pamoja nao. Kwa Mungu hii miili haina thamani hata kidogo. Chenye thamani ni roho.
 
Mungu angekuwa anababaishwa na mwili asingeruhusu Shetani autese mwili wa Ayubu kiasi chote kile isipokuwa roho yake, wala tusingekuwa tunateseka, wala watoto wadogo wasingekuwa wanakufa, wala watu wasiokuwa na hatia wasingekuwa wanakufa vitani au katika majanga mengine yoyote yale katika dunia hii.

Lakini jibu lipo, katika kitabu cha Ayubu 40:1-24, lakini hakuna atakayelielewa.

Mungu anayezungumzwa ni Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, Anayeruhusu maovu yatendeke kwa sababu ya dhambi mbili za asili: Kiburi na Zinaa. Kiburi ni dhambi ya Ibilisi. Zinaa ni dhambi ya wazazi wetu wa kwanza. Hivyo, kila kinachofanyika kimo ndani ya mpango mkuu wa Mungu wa ukombozi wa dunia hii.
 
Kila mtu kabla ya kuzaliwa alipewa na Mwenyezi Mungu unabii na nyota ya ufalme. Una bahari ya fursa ya kuwa kitu chochote unachotaka kuwa katika dunia hii. Kama unataka furaha, furaha iko ndani yako. Kama unataka utajiri, utajiri uko ndani yako. Kama unataka amani, amani iko ndani yako. Kama wewe ni tone na fursa ni bahari, wewe ni bahari ndani ya tone.
 
Amiin [emoji120][emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unabii ni uwezo alionao mtu wa kuongea mambo matakatifu ya Mungu, kuwaongoza wenzake katika njia njema. Mungu humwambia nabii kitu cha kusema na nabii huwambia wenzake kile ambacho Mungu amemwambia aseme. Mungu hawezi kuongea na watu mpaka watu wajue jinsi ya kuongea naye, na wakati mwingine ni rahisi sana kusikia ujumbe kutoka kwa mtu kuliko kuusikia ujumbe huo moja kwa moja kutoka kwa Mungu.
 
Mungu anaweza kukwambia useme kitu fulani kwa mtu au watu fulani. Unaweza usijue kwa nini anakwambia ufanye hivyo, lakini utajisikia msukumo wa hali ya juu wa kutangaza ujumbe uliopewa kuuwasilisha. Mungu hatakulazimisha, lakini atakung’ang’aniza, na ni Mungu pekee anayejua lengo la mawasiliano hayo. Mungu akikwambia ufanye kitu fanya mara moja, usiulize kwa nini.
 
Kazi yako ni kufanya unachotakiwa kufanya, kusema unachotakiwa kusema, si kuuliza maswali. Mtumie rafiki yako wa kiroho kukuongoza katika mema na mabaya, na usitambe – kwamba unaongea maneno uliyoambiwa na Mungu uyaongee. Ukiwa na uwezo mkubwa wa kuongea na Mungu utaleta mabadiliko katika dunia.
 
Mungu humwambia mtu kitu cha kusema na mtu huwambia wenzake kile ambacho Mungu amemwambia aseme. Lakini utajuaje kama Mungu amekuchagua wewe kusema au kufanya kitu? Mungu atakwambia kupitia Roho Mtakatifu, na utajisikia msukumo mkubwa wa kusema au kufanya kile ambacho Mungu anataka useme au ufanye. Unabii unaweza kumtokea mtu yoyote, mahali popote, anayejua jinsi ya kuwasiliana na Mungu.
 
Nyota ni kipaji, kipawa, takdiri, karama, au uweza; ni kiashiria cha rohoni kinachoonyesha mtu atakuwa nani baadaye, mafanikio ya mtu, au takdiri ya maisha ya mwanadamu. Unabii na nyota ya ufalme ni kibali cha Mungu katika maisha ya mtu. Kupata kibali hicho, tembea na watu sahihi katika maisha yako (tembea na watu ambao Mungu amekuchagulia kushika funguo za takdiri ya maisha yako).
 
Tamka na kukiri kibali cha Mungu katika maisha yako yote. Panda mbegu za kibali cha Mungu katika udongo wa maisha yako. Jifunze kutenda mema bila malipo, kwani wema ni mbegu ya kibali cha Mungu. Jali mambo ya ufalme wa Mungu.

Wengine hatuishi kama wafalme kwa sababu ya nguvu za giza – zilizopo kati ya Mungu na wanadamu. Nyota zetu zimefunikwa. Una kila kitu unachotafuta, ndani ya moyo wako. Usitafute furaha, utajiri au amani nje ya moyo wako. Tafuta furaha, utajiri au amani ndani ya moyo wako.
 
Usalama wa Taifa ni akili si ukali. Kazi yake, au wajibu wake; ni kukusanya, kuchanganua, kudurusu na kuunganisha kwa makini, taarifa nyeti za kijasusi za ndani na nje ya nchi kuilinda Tanzania na watu wake. Ukitaka kuwa na akili kuwa kawaida. Ukitaka kuwa na nguvu kuwa mkarimu. Ukitaka kuwa tajiri kuwa tajiri wa unyenyekevu.

Kama una akili kuwa kawaida. Kama una nguvu kuwa mkarimu. Kama una pesa kuwa mnyenyekevu. Ukitaka kuwa na akili kuwa kawaida. Ukitaka kuwa na nguvu kuwa mkarimu. Ukitaka kuwa na pesa kuwa mnyenyekevu.
 
Tunaumbwa kwa mfano wa Mungu kupitia shida na raha, kwa sababu ya ukaidi wa asili yetu kama binadamu. Bila shida na raha hatutakomaa wala hatutakamilika. Wakati mwingine Mungu anatufinya ili tusikie.

Ukaidi ni asili ya binadamu. Si rahisi kuibadili, hadi ujue wewe ni nani na kwa nini ulizaliwa. Ukijua wewe ni nani na kwa nini ulizaliwa utaishi sawasawa na mapenzi ya Mungu kwa binadamu.

Wenye shida katika Bwana wamebarikiwa. Wenye furaha ni wale wasiokuwa na furaha.
 
Kidunia wenye furaha ndiyo tunaosema wamebarikiwa. Lakini Kimungu wenye furaha ni wale wasiokuwa na furaha kwa sasa, lakini wenye hakika ya kuwa na furaha kwa baadaye. Yaani, kidunia wenye shida katika Bwana ndiyo tunaosema wamebarikiwa. Fungua moyo wako, ili uwe mkunjufu na mnyenyekevu.

Chochote kinachotokea katika maisha yako Mungu anakupa njia ya kufika pale anapotaka ufike. Jifunze lugha ya maisha ambayo Mungu anajaribu kuongea na wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…