Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mustafi amekuwa na nyakati zenye mambo tofauti huko Arsenal, akikumbana na lawama nyingi kutoka kwa mashabiki kutokana na makosa yake ambayo amekuwa akifanya, wakati Perez alicheza mechi 11 tu za Ligi Kuu England akiwa na jezi za wakali hao wa Emirates kabla ya kurudishwa kwa mkopo Deportivo na baadaye kuuzwa jumla West Ham United.
 
Cagigao, ambaye aliichezea Arsenal ya watoto chini ya Pat Rice, amekuwa msaka vipaji kwenye kikosi hicho kwa zaidi ya mika 23, ndiye aliyetoa mapendekezo ya usajili wa mastaa Cesc Fabregas, Hector Bellerin,Robin van Persie na wa hivi karibuni wa Gabriel Martinelli.
 
Lakini, kwenye usajili wa Mustafi na Perez, mabosi wa Arsenal walipuuza ushauri wake na kwenda kuwasajili wachezaji hao, licha ya kwamba waliambiwa hawana kiwango na vigezo vya kwenda kuvaa jezi za Washika Bunduki hao wa London.
 
Back
Top Bottom