Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Lakini mchezaji huyu linapokuja suala la Timu ya Taifa ya Ufaransa, hakuna utakachosema kwa kocha mkuu wa kikosi hicho, Didier Deschamps akakuelewa. Amekuwa ni chaguo la kwanza kwake licha ya kuwa ni mchezaji anayeonekana kuwa na kiwango cha kawaida kwenye klabu yake. Mpaka sasa Giroud amefunga mabao saba tu kwenye michezo 49 akiwa na Chelsea lakini ajabu amefunga mabao 39 katia michezo 97 akiwa na Timu ya Taifa ya Ufaransa na kwa sasa anashika nafasi ya tatu kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa Ufaransa akizidiwa na Michel Platini na Thierry Henry tu.
 
4.Danny Welbeck

Hapa unaweza ukashagaa kidogo je, unakumbuka Muingereza huyu ambaye aliwahi kukipiga Manchester United alishawahi kuwatupa mbali mastraika hatari kabisa kwenye kizazi hiki yaani Cristiano Ronaldo na Lionel Messi. Ndio hili lilijiri kwenye michezo ya kufuzu michuano ya Euro 2016 Walbeck ndiye aliyefunga mabao mengi kuliko Ronaldo, Eden Hazard, Diego Costa na Robin van Persie.
 
3.Andre Silva

Kama ulikuwa hujui kwenye Kombe la Dunia mwaka 2018 kule Urusi huyu ndiye aliyekuwa mchezaji aliyechangia jumla ya asilimia 70 na kuifanya Ureno ifuzu kwenye michuano hiyo. Katika kampeni hizo Andre Silva alifunga jumla ya mabao manane. Wakati mchezaji huyu anaonyesha maajabu haya ya kuibeba Ureno hali ya kiwango chake kwenye klabu ya Sevilla ambapo alikuwa anacheza kwa mkopo ilikuwa hairidhishi kabisa. Lakini moto ambao aliuonesha kwenye timu yake ya taifa ulikuwa ni hatari sana. Mpaka sasa amefunga mabao 15 katika michezo 34 ya timu ya taifa aliyocheza.
 
2.Michy Batshuayi

Michy Batshuayi alijiunga na Chelsea 2016 baada ya kuonesha kiwango bora sana akiwa kule Ubelgiji na Ufaransa, lakini tokea ajiunge na klabu hiyo amekuwa na kiwango kibovu sana mpaka ikapelekea kutolewa kwa mkopo. Pamoja na kiwango kibovu akiwa na Chelsea lakini linapokuja suala la timu ya taifa, Batshuayi amekuwa na kiwango cha kustaajabisha kwelikweli.
 
1.Javier Hernandez

Jina Javier Hernandez ‘Chicharito’ huwa linatajwa tofauti sana na wakazi wa nchi ya Mexico. Wakati barani Ulaya Chicharito akionekana kama ni straika wa kawaida, kwao Mexico anatajwa kama ni mmoja kati ya mastraika bora. Chicharito amecheza klabu kadhaa barani Ulaya lakini hakuna sehemu aliyowahi kutajwa kama ni straika bora kwenye klabu hizo. Staa huyo amezichezea Manchester United, Real Madrid, Bayer Leverkusen, Sevilla Westham United na sasa yuko LA Galaxy
 
Kwenye ngazi ya timu ya taifa amefunga jumla ya mabao 52 katika michezo 109, ukitaka kujua hatari ya huyu mwamba nenda kaulize alichowahi kuzifanya Portugal, Croatia, Italy, Argentina, Brazil, Hispania, Uholanzi na Argentina ambazo ziliwahi kujeruhiwa vilivyo na mchezaji huyu.
 
Ni balaa zito. Kuna orodha kibao za mastaa wa maana ambao thamani zao sokoni zime-shuka kutokana na janga hilo la corona, ambalo limezitikisa kiuchumi klabu kibao duniani, huku Kylian Mbappe akiwa mche-zaji pekee kwenye orodha ya masupastaa, ambaye tham-ani yake anakaribia Euro 200 milioni.
 
Kwa mujibu wa transfermarkt.com, mastaa kibao tha-mani zao zimeshuka ambapo sokoni kwa sasa bei ya supastaa wa Barcelona, Lionel Messi ni Euro 112 milioni tu.Staa wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho anayewindwa na timu kibao ikiwamo Man-chester United, thamani yake sokoni kwa sasa im-etajwa kuwa ni Euro 117 milioni, wakati mchezaji Kevin De Bruyne wa Man-chester City, am-baye thamani yake ilipaswa kuwa Euro 200 milioni, soko kwa sasa linamtam-bua kuwa na thamani ya Euro 120 milioni.
 
Straika wa Tottenham Hotspur, Harry Kane, ambaye aliripotiwa kwamba bosi wa timu hiyo Daniel Levy yupo tayari kuwauzia Man United kama watakwenda na Pauni 200 milioni, kwa mujibu wa Transfermarkt, fowadi huyo Mwingereza thamani yake sokoni kwa sasa ni Euro 120 milioni, sawa na anavyothaminishwa staa wa Liverpool, Mohamed Salah na mshambuliaji mwenzake huko Anfield, Sadio Mane, naye akiripotiwa kuwa na thamani ya Euro 120 milioni.
 
Supastaa wa Paris Saint-Germain, Neymar, ambaye ali-naswa kwa Euro 222 milioni aliposajiliwa kutoka Barcelona, thamani yake kwa sasa sokoni inatajwa kuwa ni Euro 128 mil-ioni, sawa na anavyo-thaminishwa staa wa Man City, Raheem Sterling kuwa na kiwango hicho cha thamani ya Euro 128 milioni sokoni kwa sasa.
 
Fowadi Mfaransa, Kylian Mbappe anayekipiga PSG, ndiye pekee ambaye thamani yake imebaki juu, ikikaribia Euro 200 milioni licha ya kutokea kwa janga hilo la virusi vya corona, ambapo kwa mu-jibu wa Trans-fer-markt, tham-ani ya mche-zaji huyo soko-ni kwa sasa ni Euro 180 milioni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…