Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Virutubisho

Binzari ni moja ya mmea wenye utajiri wa virutubisho vingi mno. Yasemekana, kutokana na USDA, binzari ina kiasi kizuri cha protein, vitamin C, calcium, iron (madini joto), nyuzi nyuzi (dietary fiber), sodium, na kalori 24 kwenye kijiko kimoja cha mezani chenye unga ya binzari. Pia inachangia utoaji mkubwa wa vitamin B6, potassium, magnesium, na manganese.
 
Faida kuu za kiafya za binzari na curcumin ni kama zifuatazo:1. Anti-InflammatoryTabia au sifa ya kitu kuzuia hali ya uvimbe isitokee.Binzari, kutokana na uwepo wa curcumin, inafanya kazi kama wakala wa kuzuia uvimbe kwenye mwili (anti-inflammatory agent), wanasema watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Arizona, Tucson, USA. Kiukweli hata kiasi kidogo tu cha binzari kinaweza kupunguza uvimbe wa hemorrhoids.
 
2. Utunzaji wa Ngozi

Binzari husaidia kuweka ngozi yako kwenye afya kwa namna nyingi.Huondoa chunusi kwa kuzuia bakteria wanaosababisha chunusi na kupunguza uzalishwaji wa mafuta na tezi za mafuta kwenye ngozi (sebaceous glands)
 

Watu wenye magonjwa ya moyo huwa wanashauriwa kuitumia sana na kama wasipoweza kuipata basi watumie supplements. Kachupa kadogo ka vidonge vyake au maji huuzwa kwa dola 37 madukani.
 
2. Utunzaji wa Ngozi

Binzari husaidia kuweka ngozi yako kwenye afya kwa namna nyingi.Huondoa chunusi kwa kuzuia bakteria wanaosababisha chunusi na kupunguza uzalishwaji wa mafuta na tezi za mafuta kwenye ngozi (sebaceous glands)
 
Utajiri wa Viondosha Sumu

Curcumin inayopatikana kwenue binzari ni wakala mkubwa wa kuondosha sumu ambayo husaidia kwa namna nyingi ikiwemo faida zake nyingi za urembo na tiba. Somo lililofanyika na watafiti kwenye chuo kikuu cha Edinburgh, iliichapa makala kwenye jarida la 'the Antioxidants & Redox Signaling', iliyoangazia umuhimu wa kazi ya uondoshaji sumu wa curcumin
 
Kupunguza UzitoKiungo cha dhahabu, binzari, husaidia kasi ya hufanyaji kazi wa mfumo wa chakula na kusaidia mwili wako kuunguza kalori nyingi, kitendo kinachopelekea kupunguza uzito. Ina saidia pia kwenye kupunguza mafuta yaliyoganda na kusaidia Ini kuondoa sumu, ambavyo ni vitu vya muhimu sana linapokuja swala la jitihada ya kupata 'diet' ya kupunguza uzito. Pia, na curcumin, binzari inaweza kuwa kirutubisho muhimu kwa kupunguza uzito kwani kinashusha kiwango cha LDL (Cholesterol mbaya). Pia ina wajibika vilivyo kwenye kuzuia taarifa za vivimbe kwenye misuli, kongosho, na seli za mafuta. Kwahiyo, kipindi mwili wako haupambani na uvimbe, kwa urahisi binzari inaweza kufocus kwenye kupunguza uzito kirahisi
 
Huboresha Afya ya Ini

Binzari na kampaundi zake muhimu za asili zilizosheheni zimegundulika kuimarisha ufanyaji kazi wa ini na kupunguza kiwango cha sumu kwenye mwili kwa kuweka sawa mfumo limfu (lymphatic system) na kuondoa sumu kiuhakikaKutokana na tafiti iliyofanywa 2018, uwezo wa kuondoa sumu wa binzari unaweza kuwa msaada kwenye kupunguza kuharibika kwa ini na kiungo hiki kinaweza kutumika kama mbadala wa kutibu matatizo ya ini kama cirrhosis na fatty liver disease
 
Huboresha Kazi za Ubongo

Kweny matibabu ya kitamaduni, mara zote iliegemea kwenye kuongeza uwezo wa utambuzi, kuongeza umakini, na kuongeza uwezo wa kumbukumbu. Nyingi katika hizo imani za kitamaduni ziliishia kuhakikiwa na tafiti, na binzari bado inakuwa ni dawa yenye kuongeza ufanisi wa ubongo.Inaweza pia kulinda njia ya mfumo wa neva za fahamukutoka na mlundikano wa muda mrefu wa sumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…