Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Lakini pia licha ya hilo UEFA inajua iwapo Ligi hazitomalizika kwa wakati basi hata wao watakuwa na wakati mgumu kwa kuharibika kalenda yao ya msimu ujao kwani hakutakuwa na klabu shiriki kutokana na kwamba ligi bado zitakuwa hazijaisha.
 
Kufuatia hatua hiyo UEFA inataka kuwashauri wanachama wake kuanzisha mfumo wa mtoano ili kuzipata klabu zitakazoongoza msimamo wa Ligi na kufuzu kucheza UEFA na iwapo mfumo huo utaanza kufanya kazi basi klabu za Chelsea, Manchester United zitakuwa zinahusika moja kwa moja.
 
Ikiwa mfumo unaojulikana kwa jina la kiingereza kama 'points-per-game method'. Utafanikiwa kutumika pale England klabu za Liverpool, Manchester City, Leicester na Chelsea watakuwa wanafuzu kwenda UEFA na klabu za Manchester United na Sheffield United zenyewe zitakwenda Europa League, wakati Arsenal na Tottenham watakosa vyote.
 
Liverpool wanahitaji pointi sita katika mechi zake 9 ili kutangaza ubingwa huo, kwani watetezi wa ligi hiyo Manchester City wamewachwa nyuma kwa alama 25 wakishinda nafasi ya pili na pointi zao 57 wakiwa na michezo 10 mkononi ambayo hata wakishinda watafikisha alama 87 tu.
 
Wenda jaman arsenal na sisi tukawemo kwa huruma ya UEFA mana hadi nimesahau laza ya club bingwa ulaya na kiwimbo kao ka henkeni, Mungu ibariki arsenal tuludi UEFA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
Wenda jaman arsenal na sisi tukawemo kwa huruma ya UEFA mana hadi nimesahau laza ya club bingwa ulaya na kiwimbo kao ka henkeni, Mungu ibariki arsenal tuludi UEFA

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Man u tunasema Amen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…