Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Lakini ukweli ni kwamba kiwanda cha matatizo mengi tunayopitia ni sisi wenyewe. Sikatai kwamba kuna vitu vingine viko kwenye maisha yetu kwa kusababishwa na wengine lakini kwa asilimia kubwa sisi ndio wachawi wa maisha yetu
 
Akili zetu, mitazamo yetu, hisia zetu ndio chanzo cha matatizo mengi tunayopitia. Marafiki waliotuumiza ni sisi wenyewe ndio tuliowaruhusu kuja kwenye maisha yetu. Watu ambao wameharibu biashara zetu sisi wenyewe ndio tulihusika kuwaleta kwenye hizo biashara.
 
Bali tuliamua kwenda kwa akili zetu bila kujua kwamba kila kitu tunatakiwa kukitanguliza kwa Mungu na kusikiliza ushauri wa watu tunaowaamini. Na kwa sababu hiyo leo hii tunalia na kuumia bila kujua kwamba ni sisi wenyewe ndio tuliosababisha.
 
Japokuwa ndio kuna uwezekano wa uovu au laana za wazee waliopita zinaweza zikawa zinakufatilia lakini kwa asilimia kubwa chanzo cha matatizo mengi tunayopitia sisi wenyewe ndio kiwanda. Sisi wenyewe ndio tunayazalisha.
 
Kwa hiyo badala ya kutafuta nani mchawi kwenye maisha yako kwa matatizo mengi unayopitia, angalia ni wapi ulikosea, angalia ni wapi ulijiroga mwenyewe kwa kuwaleta watu ambao wameacha makovu kwenye maisha yako. Angalia ni wapi ulikosea ukasababisha hicho kinachokusumbua leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…