Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kocha Ole Gunner Solskjaer bado anahitaji saini yake. Sambamba na hilo, Haaland anaweza kuziingiza pia kwenye vita klabu za Manchester City na Liverpool ambapo zitachuana kuwania saini yake kama zitapoteza washambuliaji wao tegemeo kwenye vikosi vyao.
 
TIMO WERNER

Fowadi huyo matata kabisa wa Kijerumani amekuwa akihusishwa na mpango wa kwenda kujiunga na Liverpool kwa miezi kadhaa sasa. Lakini, taarifa za kutoka Ujerumani zinadai Liverpool wameomba kupatiwa muda zaidi kabla ya kukamilisha dili la kumnasa mshambuliaji huyo anayethaminishwa kuwa wa Pauni 52 milioni. Ukiwaweka kando Liverpool wanaomtaka fowadi huyo wa RB Leipzig, wababe wengine wa Ligi Kuu England nao wamewekwa kwenye orodha ya kuwania saini yake jambo linalodaiwa litasababisha upinzani mkali kwenye kuinasa saini yake mwishoni mwa msimu huu wakati dirisha litakapofunguliwa.
 
DAVID ALABA

Kocha wa Chelsea, Frank Lampard ameripotiwa kuingia sokoni kujaribu kusaka beki wa kushoto wa kuja kuchukua mikoba ya Emerson.Mbrazili huyo amemfanya kocha Lampard kutokuwa na amani juu ya uwezo wake wa ndani ya uwanja na beki wa kushoto mwingine, Marcos Alonso, naye amekuwa wa nyongeza tu.
 
Kutokana na hilo, Chelsea inapiga hesabu za kwenda kuvamia Bayern Munich kunasa huduma ya Alaba, ambaye pia anaweza kucheza nafasi nyingine nyingi ndani ya uwanja ikiwa ni pamoja na kiungo wa kati na beki wa kati, kitu kitakachompa Lampard machaguo mengi kwenye namna ya kumtumia atakapotua kwenye kikosi chake.
 
MANUEL NEUER

Chelsea wanahusika kwenye mpango wa kumnyakua kina namba moja wa Ujerumani, Manuel Neuer ili kuja kuchukua mikoba ya Kepa Arrizabalaga.

The Blues wamepata matumaini makubwa ya kumnasa Neuer baada ya Bayern Munich kuripotiwa kwamba wamefuta mpango wa kumpa mkataba mpya wenye pesa nyingi baada ya kutoa maneno ya kuikosoa timu hiyo.
 
Neuer aliripotiwa kutaka mkataba wa miaka mitano kitu ambacho Bayern Munich imeonekana kukigomea na hapo ndipo panapoipa uhakika Chelsea watakwenda kunasa huduma ya kipa huyo mwenye uwezo mkubwa anaposimama golini. Chelsea walimsajili Kepa kwa pesa nyingi sana.
 
Mkataba wake utafika tamati Juni 30 na kuna klabu nyingi zimekuwa zikifukuzia saini ya staa huyo wa zamani wa kimataifa wa Ujerumani. Taarifa zinaweka wazi Gotze kwenye dirisha lijalo linaweza kumaliza kiu yake ya kwenda kujiunga na moja ya klabu zinazotamba kwenye Ligi Kuu England.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…