Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wakati ligi zikiwa bado hazifahamiki zitamalizika lini, ili kufanya dirisha la usajili kufunguliwa kuna orodha ya mastaa kibao wanaotamba kwenye Bundesliga wanaripotiwa kwamba msimu ujao huenda wakaenda kuliamsha dude huko kwenye Ligi Kuu England.
 
Usiku wa matunda
FB_IMG_1589045439739.jpeg
 
Manchester United kwa muda mrefu imekuwa ikitajwa kusaka saini ya kinga huyo wa Kingereza, Jadon Sancho ili akakipige huko Old Trafford. Man United wanamtaka Sancho akacheze pamoja na Marcus Rashford kwenye safu ya ushambuliaji ili kuwafanya kuwa moto zaidi msimu ujao.
 
Lakini, Borussia Dortmund inadai mchezaji huyo anauzwa kwa ada inayozidi Pauni 100 milioni na haipungui jambo linalozifanya klabu nyingi za Ligi Kuu England kuwa kwenye wakati mgumu wa kunasa saini yake kutokana na kukumbwa na ukata uliosababishwa na janga la virusi vya corona.
 
DAYOT UPAMECANO


Beki wa kati Mfaransa, Dayot Upamecano amekuwa akihusishwa na klabu za Manchester United na Arsenal karibu kwa miezi kadhaa sasa. Kwa kipindi cha karibu zaidi, Arsenal chini ya kocha Mikel Arteta ndio ambao wamekuwa wakihusishwa na mchezaji huyo na miamba hiyo ya Emirates inajaribu kutafuta wachezaji wa kuja kuimarisha safu yao ya ulinzi.
 
KAI HAVERTZ

Kiungo mchezeshaji wa Bayer Leverkusen, Kai Havertz amezivutia timu nyingi za Ligi Kuu England kuanzia Manchester United, Liverpool na sasa Chelsea. Kocha wa Chelsea, Frank Lampard baada ya kunasa saini ya kiungo wa Ajax, Hakim Ziyech amekuwa bize kusaka saini ya wachezaji wa safu ya ushambuliaji na hapo anampigia hesabu Havertz. Lakini, mchezaji huyo yupo kwenye mipango ya Liverpool na Man United, ambao wanahaha pia kunasa saini yake. Klabu nyingine ya nje ya Ligi Kuu England inayohitaji saini ya Havertz ni Bayern Munich na ni kama kawaida yao ya kuhakikisha wanasajili wachezaji wote wanaotamba na timu nyingine kwenye Bundesliga.
 
PHILIPPE COUTINHO

Mbrazili, Coutinho hana jipya asilolifahamu kwenye Ligi Kuu England baada ya kucheza kwa kiwango kikubwa sana alipokuwa katika kikosi cha Liverpool. Aliondoka kwenda Barcelona, Januari 2018, lakini huko mambo yake yalikuwa hovyo na hivyo kujikuta akitolewa kwa mkopo kwenda Bayern Munich anakocheza msimu huu.
 
PHILIPPE COUTINHO

Mbrazili, Coutinho hana jipya asilolifahamu kwenye Ligi Kuu England baada ya kucheza kwa kiwango kikubwa sana alipokuwa katika kikosi cha Liverpool. Aliondoka kwenda Barcelona, Januari 2018, lakini huko mambo yake yalikuwa hovyo na hivyo kujikuta akitolewa kwa mkopo kwenda Bayern Munich anakocheza msimu huu.
 
ERLING HAALAND

Manchester United ilijaribu kumsajili straika Haaland kabla ya kinda huyo kunyakuliwa na Borussia Dortmund kwenye dirisha la Januari mwaka huu. Lakini, kila kitu ndio kwanza kama ndio kimeanza kutokana na ukweli kwamba Man United bado wanafukuzia saini ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Norway.
 
Back
Top Bottom