Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ulizaliwa Uishi Wewe, Usiishi Kwa Ajili Ya Wengine.
Kila mtu alivyoumbwa kuna kitu alizaliwa ili aje kukifanya, analo jibu la changamoto fulani katika maisha haya tulimo. Ni wajibu wa kila mmoja kuweza kutambua hilo na kuishi hilo kusudi. Hakuna hata mtu mmoja aliyezaliwa ili aje kuwa kama mtu mwingine, ulizaliwa uwe wewe. Kila mtu ni wa pekee ana uwezo wa kufanya mambo kwa namna yake ambayo hakuna mwingine anaweza kufanya hivyo.
 
Kuna mwingine amezaliwa kufundisha wengine tu, popote alipo ualimu wake utaonekana tu, yaani atafurahia kufundisha tu hata kama hamna kipato anapata lakini yeye kuna amani anaipata ndani mwake, kuna kile kitu unaweza kufanya bila kutanguliza malipo, kile ambacho usipofanya unasikia kama una deni, unaona haujatimiza wajibu wako sawasawa. Ukishagundua kusudi la wewe kuwepo ni wajibu wako wewe mwenyewe kulisimamia na kuliishi hilo, ukimshirikisha Muumba wako katika kila hatua.
 
Pengine baada ya kugundua kusudi lako ni lipi, unaweza kukutana na vikwazo vingi katika kuliishi hilo kusudi. Ndugu yangu tambua kwamba ni wewe na Mungu wako mnaelewa hilo kusudi hivyo usitegemee kila mtu akuelewe kirahisi, usishangae kuona uliotegemea wakuelewe wasipokuelewa. Na hiyo isiwe sababu ya wewe kuona labda umepotea au hauko sawasawa,
 
kuna maisha ya mtu yanaguswa na kumfanya awe mtu bora zaidi, na ndiyo furaha yangu hiyo.
Hivyo haijalishi unakutana na nini, naomba kama kweli una uhakika ndicho kitu umeitiwa endelea kufanya, ng’ang’ana tu wapo watakaokuelewa baadae, kuna watu mtoto akizaliwa wanashindwa kuelewa kama anafanana na nani lakini kadri anavyoendelea kukua
 
Wakati mwingine hata mzazi anaweza kukutaka uwe mtu fulani kwa sababu zake binafsi na pengine nzuri tu. Mwingine anaweza kukutaka ufanye kitu fulani kwa manufaa yake. Ishi wewe vile ulikusudiwa kuwa, tumia hekima na busara kuwaelewesha wanaotaka uwe tofauti na ulivyo wakati wewe una uhakika hivyo ndivyo unavyopasa kuwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…