Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Tupo hapa kujifunza na dunia ndiyo mwalimu wetu.Maisha ni mwendelezo wa masomo, kila changamoto unayokutana nayo kwenye maisha ni somo unalopaswa kujifunza kwenye maisha yako. Ukitatua changamoto hiyo unakuwa umefaulu somo hilo na hivyo kwenda ngazi ya juu zaidi, kupata changamoto kubwa zaidi. Ukishindwa kutatua utaendelea kupata changamoto hiyo hiyo, hivyo utarudia somo hilo mpaka ufaulu.