Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kila kitu kinachotokea kwenye maisha kinatokea kama kinavyopaswa kutokea. Jukumu lako ni kuona unakitumiaje ili kupata kile unachotaka wewe, na siyo kupingana nacho au kukataa, kwa sababu kadiri unavyopingana nacho, ndivyo unazidi kukikuza, na mwisho wa siku maisha yatashinda.
 
Usijaribu kukimbizana na kila kitu kwenye maisha, huwezi kufanya kila kitu, chagua kufanya yale muhimu na pata muda wa kufurahia maisha yako. Ukifa leo dunia haitasimama, kila kitu kitakwenda vizuri kabisa bila ya wewe. Hivyo ishi vizuri, furahia maisha na chukulia kila kinachotokea kwenye maisha yako kama sehemu ya maisha na siyo kizuri wala kibaya.
 
Njia ya kuwapenda watu ni kuwakubali kama walivyo.
Ukishaanza kusema unawapenda watu kwa sababu wako kwa aina fulani, na ukishaanza kutaka watu wabadilike na kuwa kama unavyotaka wewe ndiyo uwapende, jua hapo hujawapenda watu. Haitatokea kila mtu kwenye maisha yako kuwa kama unavyotaka wewe. Na watu hawatabadilika kwa namna unayotaka wewe.
 
Dhumuni lako kwenye maisha siyo kuibadili dunia, bali kujibadili mwenyewe.
Ni rahisi sana kusema unataka kuibadili dunia, lakini hilo ni jambo ambalo huwezi kulifanya. Dunia haihitaji msaada wako kwenye kuibadili, dunia iko sawa kwa namna ulivyo. Wewe ndiye unayehitaji msaada wa kubadilika, hivyo jukumu lako kubwa ni kujibadili wewe mwenyewe.
 
Jua ni kitu gani unachohitaji kwenye maisha yako na fanyia kazi kukipata, hicho ndiyo kitakuhitaji wewe kubadilika, kitakuhitaji wewe uwe bora na kuweza kufanikiwa zaidi. Usikazane kubadili dunia, kazana kujibadili wewe mwenyewe na dunia itakuwa bora sana kwako.
 
Katika mambo haya 10 tuliyojifunza, hakuna hata moja linalokutaka wewe uwe na elimu kubwa, uwe na fedha nyingi au uwe na rangi fulani kwenye ngozi yako. Yote ni mambo ambayo mtu unaweza kuchagua kuyaishi wakati wowote wa maisha yako na maisha yako yakawa rahisi, ukaacha kuyafanya kuwa magumu zaidi.
 
Tuchukue mfano mdogo, kuna wafanyabiashara wawili, wote wanafanya biashara ya aina moja na kwenye eneo moja. Mmoja huwa anafungua biashara yake saa moja kamili asubuhi na kufunga saa tatu kamili usiku, kila siku bila ya kuacha. Mwingine hana muda maalumu wa kufungua wala kufunga, lakini mara nyingi huwa anafungua saa mbili asubuhi na kufunga saa kumi na mbili jioni. Kama hakuna kingine kitakachobadilika, kama huduma wanazotoa ni sawa, unafikiri miaka mitano ijayo yupi ambaye atakuwa amepiga hatua zaidi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…