DODOMA :- *SPIKA NDUGAI: MBOWE HARUDI BUNGENI NOVEMBA, WABUNGE WALIOFUKUZWA UANACHAMA WAENDELEE KUHUDHURIA BUNGENI KAMA KAWAIDA
Spika wa bunge Job Ndugai amewaambia wabunge wote wa CHADEMA waliofukuzwa uanachama waendelee kuhudhuria vikao vya bunge kwa kuwa hakuna kosa lolote la kisheria walilolifanya
Amesema "wabunge wanaapishwa na spika, na ninyi karibia wote nimewaapisha Mimi, hakuna cha nini wala nini, na vikao hivyo vya majungu hivyo havifanyi kazi, eti mtu mmoja katika nchi hii anajifanya anamamlaka ya kufukuza wabunge anavyotaka"
"Sijui anafanya hivyo kwa kuwa ameona mwezi Novemba hawezi kurudi hapa bungeni anaona awaharibie na wenzake, haiwezi kuwa sawa" amesema Spika Ndugai
Sikieni ndugu zangu, nyie wabunge wote humu ndani niliwaapisha mimi, na mimi sijatengua ubunge wenu. Hakuna wa kuwaondolea ubunge wenu mpaka nitakapoidhinisha. Na haiwezekani mtu mmoja ajione ana mamlaka ya kuamua anavyotaka. Hicho kikao chao ni batili. Yani watu kuhudhuria bungeni tu liwe kosa la kufukuzwa Haiwezekani.
Wananchi wanachagua mbunge sio ili awe chini ya mtu fulani. Kwamba akijisikia kuwapeleka hivi au vile wafuate tu. Mara kwenye mishahara yenu leteni kiasi fulani kwangu. Mara msiingie bungeni, yani mtu mmoja tu anajiona ana mamlaka ya kufanya anayotaka? Tulieni hakuna cha kimkutano wala kikao kinachotambulika kisheria kuwavua ubunge wenu" Bwana Job Ndugai,
11/05/2020.