Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Afisa anayekatisha tiketi amefariki baada ya kutemewa mate na mwanaume mmoja anayedaiwa kuwa alikuwa na maambukizi ya virusi vya Covid-19.
Belly Mujinga, 47, ambaye alikuwa na matatizo ya kupumua, alikuwa akifanya kazi katika kituo cha Victoria jijini London mwezi Machi alipodhalilishwa, sambamba na mfanyakazi mwenzie wa kike.
Ndani ya siku kadhaa baada ya tukio hilo, wanawake wote waliugua ugonjwa wa Covid-19
 
Polisi wamesema kuwa madai yamefunguliwa ili kumtafuta mwanaume aliowatemea mate wanawake hao wawili.
Bi. Mujinga alikuwa kwenye kituo hicho tarehe 22 mwezi Machi wakati alipokabiliwa na mshukiwa huyo.
Mumewe Lusamba Gode Katalay alisema mwanaume huyo alimuuliza mke wake alikuwa akifanya nini pale.
''Alimjibu alikuwa kazini pale na mtu huyo akasema ana virusi kisha akamtemea mate,'' aliongeza.
 
Bibi Mujinga alilazwa hospitali ya Barnet tarehe 2 mwezi Aprili na kuwekwa kwenye mashine ya msaada wa kupumua. Lakini alifariki siku tatu baadae, Shirikisho la wafanyakazi wa usafirishaji (TSSA) lilisema.
Msemaji wa ofisi ya Waziri Mkuu amelielezea shambulio hilo dhidi ya mfanyakazi wao muhimu ni ''la dharau''
 
Bwana Katalay alisema alimpigia simu mkewe kwenye programu ya video alipokuwa hospitalini, lakini hakusikia kutoka kwake tena.
"Nilidhani anaweza kuwa amelala, lakini daktari alinipigia simu kuniambia kuwa amefariki," alisema.
"Alikuwa mtu mzuri, mama mzuri, na mke mzuri. Alikuwa mtu anayejali na angemtunza kila mtu."
 
Watu kumi walihudhuria mazishi ya Bi Mujinga, pamoja na binti yake wa miaka 11.
Binamu yake Agnes Ntumba aliiambia BBC kuwa Bi Mujinga anaamini yuko salama katika mazingira yake ya kawaida ya kazi .
"Haipaswi kumfanya afanye kazi kwenye msongamano huo," alisema.
"Hangekuwa amekufa katika hali hii. Tungeweza kuyazuia - ikiwa angekuwa na PPE zaidi au ikiwa wangemweka ndani badala ya kuwa kwenye sehemu ya wazi''
 
Kadi nyekundu nyingi zaidi zilitolewa katika mchezo wa timu hasimu Claypole na Victoriano Arenas kutoka nchini Argentina mwaka 2011. Refa alitoa kadi nyekundu 36 zikienda kwa wachezaji wote, wachezaji wa akiba na makocha wa timu zote mbili.
 
Roman Abramovich aliinunua Chelsea kwa Tsh Bilioni 398 mwaka 2003 na kuweka rekodi ya kutumia pesa nyingi zaidi kununua klabu katika historia ya mpira duniani.


Kumbuka Neymar na Mbappe wameuzwa kwa zaidi ya Tsh Bilioni 569.
 
Tafiti: Watoto wa kwanza kuzaliwa huwa na akili zaidi ukilinganisha na watoto wanaofuatia sababu mojawapo ikitajwa ni kutokana na kupata mchango mkubwa zaidi kutoka kwa wazazi kipindi cha ukuaji tofauti na wanaofuatia.

Chanzo: Webmd
 
Bijagos Archipelago ni jamii inayopatikana Guinea Bissau, wao Mwanamke ndie mwenye mamlaka zaidi ambapo huchagua mme anaemtaka, humiliki mali na shughuli zingine huwa maamuzi yote huanzia kwa mwanamke.Wanaume huvaa vizuri ili kuwavutia wanawake,
 
Kusini mwa Malawi, Wanaume hukodiwa na kulipwa kufanya mapenzi na mwanamke aliyetoka kufiwa na mme wake kwa kile kinachodaiwa kuondoa mikosi na roho chafu katika familia nzima. Tamaduni hiyo inaitwa "Fisi" na wanaume hao huitwa "Mafisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…