Yuya na Tuya ilikuwa ni familia yenye hadhi ya juu huko misri (misri ya zamani) ambao waliishi katika miaka ya 1390 kabla ya kuja kwa Yesu Kristo
Kupitia familia kumezaliwa kizazi cha wafalme na malkia wenye historia kubwa nchini misri
Tuya alikuwa ni mke wa Yuya na walizaa Tiye , Anen, AyTiye aliolewa na mfalme Akhenaten wakazaa Mfalme Tutankhamun
Mfalme/Pharao Tutankhamun ndio mfalme mwenye umri dogo zaidi aliyewahi kuiongoza misri. alitawazwa kuwa mfalme akiwa na miaka 9 tu.Mfalme/Pharao Tutankhamun alimuoa Dada ake wa kuzaliwa aliyeitwa Ankhesenamun (hapo awali ilikuwa ni kawaida kwa Dada na kaka kuoana katika nchi ya misri )Mengine usiyoyajua kuhusu mfalme/pharao Tutankhamen- alifariki akiwa na miaka 18- Jina lengine huitwa King Tut- kwenye mlango wa kuingia kwenye kaburi la Mfalme Tut kuliandikwa maneno KIFO KITAMPATA YOYOTE ATAKAYESUMBUA MAPUMZIKO YA MFALME TUT
Mwanasayansi Lord Carnarvon aliyeingia kwenye kaburi la Tut mwaka 1923 kwa ajili ya kufanya utafiti alifariki wiki chache baada ya kuingia humo, sababu ya kifo cha Lord Carnarvon ni kung'atwa na Mbu hata mbwa wake naye alifariki (japo hakuingia)