Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma katika dunia ya sasa tunayoishi kuna kila aina ya taarifa, matukio na mambo mengine mengi ambayo kwa pamoja katika namna fulani usipokuwa makini yanaweza kuwa moja ya vikwazo vya wewe kushindwa kufanya baadhi ya mambo ambayo ni ya msingi kazini kwako, katika familia yako, katika biashara yako na katika mambo mengine yanayohusu maisha yako kwa ujumla.
 
Ni rahisi sana kuacha kufanya jambo ambalo ulilikusudia kwa siku ya leo bila hata kujua imetokea vipi hujafanya jambo hilo lakini ukikaa kutathmini utaona sababu kubwa ni muda ambao umeupoteza kwa kufanya vitu ambavyo hukuvipanga na ambavyo si vya msingi katika kuboresha maisha yako.
 
Ni kweli mabadiliko katika mambo ambayo uliyazoea pamoja na kwamba hayana tija si jambo jepesi lakini bado inawezekana, anza kubadilisha kidogo kidogo na baada ya muda utajikuta umejenga uwezo mkubwa wa kubadilisha mambo mengi na kwa wakati mfupi
 
Back
Top Bottom