Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ni rahisi sana kuamini kuwa aina ya maisha unayoishi kwa sasa ndio kiwango cha juu cha mafanikio unayoweza kuyapata bila kujua kuwa mafanikio hayo ni sehemu ndogo tu ya uwezo wako wa ndani uliotumika huku ukiacha hazina kubwa inateketea ndani yako bila wewe kujua.
 
Kwa baadhi yetu, kama ukifanya tathmini na ukaona maisha yako hayaeleweki hayana mbele wala nyuma tambua kuwa ndani yako kuna hofu kubwa ambayo umeijenga na unaishi nayo na hofu hiyo ina nguvu kubwa kuliko imani uliyo nayo juu ya uwezo wako katika kubadili na kutengeneza maisha unayoyataka.
 
Siku ya leo sikiliza sauti zinazotoka ndani yako ambazo zimejikita katika kukukwamisha na kisha nena kwa kinywa chako kuwa kamwe hautarudi nyuma utasonga mbele kwani uwezo wa kufanya hivyo tayari uko ndani yako. Nakutakia siku njema yenye mafanikio tele.


From

Vicent Stephen.(fb)
 
IMG-20200515-WA0001.jpg
 
Back
Top Bottom